Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
- Tatizo hili haliwapati watoto wenye umri chini ya miaka miwili na huwapata zaidi watu wenye umri kati ya 15-30, huku wanaume ndiyo wanaongoza kwa kupata ugonjwa huu.
Ni takriban wiki mbili zilizopita mmoja wa wanahabari wetu wa Mwananchi alinusurika katika hatari ya kufa baada ya kupatwa na tatizo hili la kidole tumbo.
Hili lilimtokea ghafla akiwa mkoani Dodoma kwa ajili ya majukumu yake ya kawaida ya kikazi na kulazimika kufanyiwa upasujai wa dharura.
Ni mengi yameulizwa baada ya tukio hilo. Tunaposema kidole tumbo au kwa lugha ya kitaalamu appendix, tunamaanisha ni sehemu ya utumbo iliyo na umbile kama kidole na uwazi kama kijibomba inayoning'inia katika makutano ya utumbo mpana na mdogo katika sehemu ya upande wa kulia wa tumbo.
Mpaka dakika hii wanasayansi hawajui kijinyama hiki kina kazi gani, ingawa wapo wanasayansi waliowahi kusema kuwa yalikuwa ni makosa ya kiuumbaji na kwamba haikupaswa kuwepo katika tumbo.
Katika nchi zilizoendelea, wao huamua kuwafanyia upasuaji watoto wao wanapozaliwa kwa kuondolewa mapema ili kuepuka kadhia hii pale ukubwani, pia tatizo hili halijulikani ni kwa nini linawapata baadhi ya watu tu.
Tatizo hili haliwapati watoto wenye umri chini ya miaka miwili na huwapata zaidi watu wenye umri kati ya 15-30, huku wanaume ndiyo wanaongoza kwa kupata ugonjwa huu. Inaonyesha kuwa watoto wanne kati ya 1,000 walio katika umri wa miaka 14 hupatwa na ugonjwa huu na kulazimika kufanyiwa upasuaji.
Dalili za uambukizi wa kidole tumbo
Ilikuwaa ni saa nne asubuhi pale nilipoanza kujisikia maumivu upande wa kulia chini ya tumbo, yalikuwa ya ghafla na taratibu huku yakiongezeka na kuwa makali yasiyovumilika, mwanahabari wetu anaeleza.
Hata hivyo, kwa jumla dalili si lazima zijitokeze zote, lakini dalili za mwanzo zinazojitokeza ni kichefuchefu, mara nyingine kutapika, kuumia upande wachini wa kulia wa tumbo pale unapominya, maumivi sehemu ya katikati ya tumbo na unapominya sehemu hiyo maumivu huweza kusambaa na kusikia maumivu upande wa chini wa kulia, maumivu hayo huweza kuongezeka pale unaposogea, kukohoa au kupiga chafya.
Dalili nyingine ni kama vile homa na kutetemeka, kutokupata haja, kushindwa kuhimili kupitisha gesi ya tumboni kwa njia ya haja kubwa, tumbo kuvimba, kuharisha na kukosa hamu ya kula.
Basi kwa dalili hizo hapo pale unapoona dalili ni vyema kufika katika huduma za afya mapema.Tatizo hili linatibika?
Daktari anaweza kuamua endapo ulazwe au urudi nyumbani baada ya kukufanyia uchunguzi, kwa upande wa mwanahabari wetu yeye alipewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa baada ya kuonekana pana uwezekano mkubwa wa kuwa na tatizo hilo.
Tatizo hilihili halihitaji vifaa vikubwa kwa ajili ya kugundua, bali ni namna ulivyojieleza kwa daktari, baada ya daktari kukufanyia uchunguzi yakinifu wa kimwili kama vile kutomasa sehemu ya tumbo na kutumia kidole cha shahada kwa njia ya puru, ingawa vipimo kama vya uchunguzi wa damu kuangalia kama kuna uambukizi na vimelea vya maradhi, utra-sound unaweza kutumika kuona kama kidole tumbo kina uambukizi pia saa nyingine usishangae pale utakapopigwa x-ray hii inasaidia kujua kama kuna uhusiano wa tatizo na nimonia.
Baada ya mwanahabari wetu kufanyiwa uchunguzi alipewa taarifa ya kutakiwa kufanyiwa upasuaji wa dharura, ilikuwa ni taarifa ya kushtua kidogo iliyoshindwa kukubalika akilini mwake, pale alipopewa fomu maalumu ya kusaini ili kuidhinisha kukubaliana na upasuaji.
Kwanza, aligoma huku akiomba aruhusiwe tu arudi Dar es Salaam, fikra iliyojengeka kwake kuwa Jiji la Dar es Salaam ndiyo kila kitu, hospitali bora na madaktari.
Waaguzi walimwambia kama anahitaji kurudi Dar basi ni vyema akaandike maelezo kuwa anajiruhusu mwenyewe kurudi Dar, maelezo hayo yangeweza kuwaweka salama kuwa wao hawakumruhusu pale litakapotokea la kutokea.
Mwanahabari wetu alijitetea kuwa amegoma kusaini kwa sababu haelewi sababu wala hajapata maelezo ya tatizo lake ni nini, pongezi kwa daktari aliyebeba jukumu la kuchukua muda na kumwelewesha mwanahabari wetu kuhusiana na tatizo lake mpaka akaelewa na akaanguka sahihi kukubaliana na upasuji.
Kwa hili wahudumu wa afya wanapaswa kujifunza kuwapa maelezo wagonjwa wao wa tatizo linalowasumbua, ingawa katika utekelezaji wa haya kuna vikwazo vingi hasa moja kubwa ni kutokuwiana kwa wahudumu wa afya na wagonjwa, madaktari wa upasuaji ni wachache na wagonjwa ni wengi sana, utawapa maelezo wangapi? Lakini zote ni changamoto hakuna namna nikukabilina nazo.
Nini kingetokea kama mwanahabari angegoma?
Pale kidole tumbo kinapopata madhara na kupata shambulizi ya vimelea, huwa na hatari ya kupasuka wakati wowote.
Kidole tumbo kikipasuka humwaga mamilioni ya vimelea na kusababisha madhara zaidi na mgonjwa angehitaji upasuaji mkubwa zaidi na unaochukua muda mrefu zaidi, pia muda wa kukaa hospitali huwa mrefu zaidi na jeraha nalo huwa kubwa zaidi ukilinganisha na upasauji kabla ya kupasuka ambao ni operesheni ya kawaida ya appendix.
Mgonjwa anaweza kulazwa kwa muda wa saa 12-24 ili kuona kama atahitajika kufanyiwa upasuaji wa dharura.Matibabu ya appendix huhusisha upasuaji uitwao appendectomy, njia hutumika kukuondoa kidole tumbo na njia hii ndiyo ilitumika kwa mwanahabari wetu.
Kutokana na kukua kwa teknolojia ipo njia ya kisasa iitwayo laparascope, njia ambayo hurahisisha upasuaji kwani jeraha huwa dogo milimita 5-10 na huhitaji kulazwa mgonjwa hufanyiwa upasuaji siku hiyo hiyo na kurudi nyumbani.
Chombo maalum chenye kamera, kisu chenye kukata na kuchomelea mishipa ya damu isivujishe damu na kakikapu cha kubeba kidole tumbo baada ya kukatwa.chanzo.Shambulizi la kidole tumbo - mwanzo - mwananchi.co.tz