mkuu
gfsonwin , vipi hali ya mama yako? naomba utupe mrejesho please.
Nina ndugu yangu (aged 28) ananyemelewa/amepata stroke likely. Wanasema huwa ana historia ya presha ya kupanda. Juzi usiku alianguka chini (kuanguka kwa kawaida baada ya kuhisi kizungu zungu). Wakampeleka hospital, akachomwa sindano na kulazwa kwa night moja kuamkia jana, asubuhi akawa discharged akaendelee kunywa dawa nyumbani. Alipata matibabu yafuatayo:
1. Lasix - Sindao
2. Junior asprin - Vidonge
3. Olmesar H - Vidonge
4. Nifedipine - Vidonge
5. Neuroton - Vidonge
6. To attend Physiotherapy - hii bado hawajafanya.
Tangu alipodondoka ile usiku, akawa anahisi upande mmoja wa mwili (kuanzia mdomo, mkono, na mguu) una ngazi, yaani viungo hivyo upande mmoja wa mwili vimeganda! Hata kuongea hatamki maneno vizuri.
Alianza kutumia dawa hizo za vidonge jana asubuhi baada ya kuwa discharged, alikuwa hana nguvu kabisa hawezi kusimama wala kunyanyuka pekeake. Leo kaamka ana nguvu kidogo (japo bado hawezi kuinuka pekeake) na ule mguu uliokuwa umeganda/umepooza ameanza kuusense kwa mbaaali akikanyagia. Ila mkono bado kabisa umeganda (hausense kabisa) na mdomo pia bado (hatamki maneno vizuri).
Kama una chochote cha ku-share regarding kutibia mgonjwa wa stroke, nitashukuru sana.
-Kaveli-