Shamimu Mwasha na Abdul Nsembo wahukumiwa kwenda jela maisha baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha Dawa za Kulevya

Ila maisha haya, siku moja nilimuona pale karume yuko na discovery moja matata amekula glass zake nikajiuliza vile vibubu alivyokua anapromote insta vinalipa hivi?
 
Tamaa mbaya huyo demu alimuacha jamaa na mtoto wa kike akaenda kuolewa na wauza unga sasa kiko wapi?
Tujifunze kurithika na tulivyonavyo tamaa mbele mauti nyuma
Si nasikia kuwa huyo nsemo mwanzo alikua anatoka na rafiki yake shamim bdae shamim akafanya mapinduzi na ndoa juu, rafiki yake alikua host wa kipindi fulani TBC kilichokua kinadhaminiwa na mfuko mmojawapo wa hifadhi ya jamii
 
Hawa wakipaki magari kuingia misikitini wanaheshimika mpaka Sheikh anawatetemekea kwakuwa wanaingiza Swadaka na Zakat wanatoa

Wanajifanya kuona kitimoto na pombe ndio haramu ila heroine na Cocaine sio

Mijusi hii.

Kimboko by night! Hatari sana
 
Tatizo ukishabobea kwenye biashara haramu inayokuingizia pesa za kufuru unahisi unaweza kununua mamlaka zote na hata ku-earn social trust. Kuna yule mfanyabiashara wa madawa wa mexico hadi kumkamata ilikuwa shida kwa sababu kwa namna alivyokuwa anatoa misaada kwa jamiii walikuwa tayari kumlinda asikamatwe....ila mwisho wake ndo unakuwa hivyo.
 
Ubaya wa hii biashara unaweza kula na system ya wana usalama kwa kitambo kirefu mno, ila uongozi ukibadilika tu unaliwa kichwa chapu, kuna ambao walisanuliwa kuwa mambo sio wakaushe ila huyu bwana anaonesha alikuwa na asili ya kiburi
Hata yy alionywa mara kibao, wenzake wote walikimbilia south wengine wakaachana na hii mambo yy naona pressure za matanuzi na mivimbo ikamjaa, nyumba ilipigwa sachi zaidi ya masaa kumi hola mwishoni wazee wakasema ebu tuchek haya magari, wakakuta mzigo umeshonwa kwenye leather seat ya discovery.
 
Jamaa jeuri sana + dharau

Ova
 
Kabisa nashangaa watu wanamuongelea tofauti humu kama shetani fulani,kosa lake ni hilo tu kuolewa na shetani mwisho yeye nani asimlinde mume wake tuache kuhukumu tutahukumiwa....Mungu amfanyie wepesi Shamimu kwa kweli!
Amfanyie wepesi kwa kuharibu maisha ya vijana wa Huyo huyo MUNGU .

Acha zenu nyie madawa ya kulevya Ni hatari Sana kwa ustawi wa Taifa

Shamimu alikuwa anajua fika mumewe anajohusisha na hayo makitu why hakumbadilisha

Msifanye mna huruma Sana wakati kitaa tunapoteza nguvu kazi

Siku ndugu yako akiingia ulimwengu wa dawa za kulevya ndio utaelewa
 
Tatizo lako nini,nawe si umlaani kwani lazima wote tumuangalie kwa jicho lako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…