Shamira asikiliza kero za mama ntilie na bodaboda Singida ili kuzipatia ufumbuzi!

Shamira asikiliza kero za mama ntilie na bodaboda Singida ili kuzipatia ufumbuzi!

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa Viti Vitatu Bara Ndg. Shamira Mshangama ametembelea wamama wafanyabiashara ya chakula “mama ntilie” pamoja na vijana wa boda boda katika soko la Msufini Singida Mjini.

Shamira ameongozana na Mbaraza wa UVCCM Mkoa wa Singida Ndg. Amisa Msele, kamati ya utekelezaji ya mkoa pamoja na Viongozi wa Wilaya ya Singida mjini wakiongozwa na Mwenyekiti mwenyeji wa UVCCM Singida Mjini Ndg. Mohamed Msaghaa.

Ziara hio ya sokoni hapo ilikuwa na lengo la kuzungumza na wafanyabiashara hao ni kusikiliza, kutatua na kuahidi ufumbuzi wa kero zinazowakabili. Pia kuonesha jinsi UVCCM inathamini mchango wao katika kukuza na kujenga Uchumi wa Taifa.

Amewakumbusha juu ya fursa mbalimbali ikiwemo ya kuomba mikopo ya Halmshauri ya asilimia 10 iliyorudishwa hivi punde na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mwisho, amewahimiza ushiriki wao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

Shamira katika ziara hio amekabidhi eploni kwa wanawake 50 wafanyabiashara ya chakula katika kuwarahisishia katika majukumu yao.
 

Attachments

  • IMG-20241004-WA2189.jpg
    IMG-20241004-WA2189.jpg
    353.2 KB · Views: 2
  • IMG-20241004-WA2191.jpg
    IMG-20241004-WA2191.jpg
    375.2 KB · Views: 3
  • IMG-20241004-WA2193.jpg
    IMG-20241004-WA2193.jpg
    712.4 KB · Views: 3
  • IMG-20241004-WA2185.jpg
    IMG-20241004-WA2185.jpg
    383.9 KB · Views: 4
Back
Top Bottom