Shamsa Ford asema mahari yake ni Milioni 20

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368

Muigizaji wa Filamu Tanzania Shamsa Ford

Muigizaji wa Filamu Tanzania Shamsa Ford, amesema kutokana na uzuri alionao, anaamini mwanaume anayetaka kumuoa kwa sasa anapaswa kutoa mahari ya shilingi Milioni 20.

Shamsa Ford ametoa kauli hiyo katika kipindi cha KIKAANGONI, kinachorushwa kila siku ya Jumatano katika kurasa za Facebook na YouTube za East Africa TV, ambapo amesema kwa mwanaume anayetaka kumuoa aende na gari lililoandikwa 'Will You Marry Me'.

Shamsa Ford amesema kuwa "mtu akitaka kunioa sasa hivi, naangalia kwanza mfuko wake ukoja ila ninachotaka mimi siku ya kwanza kuja kunipa ombi la kunioa aje na gari lililoandikwa Will You Marry Me,"

"Unajua mimi ni ninastahili mahari zaidi ya Milioni 10 au Milioni 20 kwa sababu mimi ni mzuri, na mtu akinipata mimi maana yake amepata mtu mwenye vigezo vya kuwa mke bora, najua kupika najua kulea familia." amesema Shamsa Ford.

Aidha katika kipindi hicho Shamsa Ford, amesema hakumbuki chochote kwa aliyekuwa mume wake Chid Mapenzi wakati wakiwa kwenye mahusiano, bali anayemkumbuka ni Msanii Ney wa Mitego ambaye alikuwa na tabia ya kununa kwenye mahusiano.

Chanzo: EATV
 
Milioni 20??

Yeye anaona uzuri ndio kila kitu, huo uzuri wake mbona haujamdumisha kwa mumewe wa kwanza, huyo mumewe wa kwanza sidhani kama ilifika hata milioni 5.

Mahari hiyo bora niende zenji nikaoe hata wanawake wajane tu, najichukulia wajane wangu wa4 narudi kupyatila pyatila bongo dar es salaam
 
1. Ameshazalishwa.
2. Background ya mahusiano yake yote tunayo wananzego.
3. Kashazushiwa kuwa na ng'onda na waliokuwa nae.
4. Mfupi na mnene kiasi kwamba sehemu inayotenganisha mapaja na miguu huwezi kuiona.

Labda mababu wa kizungu ndio watatoa hiyo 10 million na wakitoa jicho ataliwa sana kama kina Lucy Komba 🤣🤣
 
Lol, milioni 20?? kwa lipi zaidi. Na kudanga kote kule kwa baadhi ya wasanii, sidhani kama hiyo milioni 20 ni halali kwake although she's a super hot lady out there, she's one of the cutest bongo movie in Tanzania.
 
Ananuka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…