beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Muigizaji wa Filamu Tanzania Shamsa Ford
Muigizaji wa Filamu Tanzania Shamsa Ford, amesema kutokana na uzuri alionao, anaamini mwanaume anayetaka kumuoa kwa sasa anapaswa kutoa mahari ya shilingi Milioni 20.
Shamsa Ford ametoa kauli hiyo katika kipindi cha KIKAANGONI, kinachorushwa kila siku ya Jumatano katika kurasa za Facebook na YouTube za East Africa TV, ambapo amesema kwa mwanaume anayetaka kumuoa aende na gari lililoandikwa 'Will You Marry Me'.
Shamsa Ford amesema kuwa "mtu akitaka kunioa sasa hivi, naangalia kwanza mfuko wake ukoja ila ninachotaka mimi siku ya kwanza kuja kunipa ombi la kunioa aje na gari lililoandikwa Will You Marry Me,"
"Unajua mimi ni ninastahili mahari zaidi ya Milioni 10 au Milioni 20 kwa sababu mimi ni mzuri, na mtu akinipata mimi maana yake amepata mtu mwenye vigezo vya kuwa mke bora, najua kupika najua kulea familia." amesema Shamsa Ford.
Aidha katika kipindi hicho Shamsa Ford, amesema hakumbuki chochote kwa aliyekuwa mume wake Chid Mapenzi wakati wakiwa kwenye mahusiano, bali anayemkumbuka ni Msanii Ney wa Mitego ambaye alikuwa na tabia ya kununa kwenye mahusiano.
Chanzo: EATV