Shamsa Mwangunga kuvaana na John Mnyika Ubungo

Hii habari nimemegewa na mwana “Kamati Ushindi” ya Mwangunga. Naishia hapa kwanza ili wabishi waje.
Hivi John Mnyika amejitangazia hati-miliki ya Ubungo, si aligombea 2005 na kushindwa. Huko Chadema hakuna wanachama wengine wakajaribu kugombea jimbo hili?
 
Mwangunga amefulia hata kama ni Mwa JF, personally naona hilo jimbo toka uchaguzi wa 2000 tumekuwa tukishinda sema hila tu za hao waroho wa madaraka, na ukitaka kujua kuwa CHADEMA ni wana democrasia na tukichukua hii nchi tutaiendesha Kidemocrasia we angalia tu majimbo yote ambayo tunashinda halafu hao mafisadi wa amadaraka wanapora tumekuwa hatuna shida, make tunajua ipo siku tutashinda.

halafu suala la tume huru sijui Viongozi hawa wa vyama kwanini wamekaa kimya, hivi mtu unategemea unaweza kujiua mwenyewe na ili mradi silaha zote na mashambulizi unazo mwenyewe, nani alikuambia mtu unaweza commit suicide with no reason behind, mimi ningeshauri bado hatujachelewa it is our time now starting to press for the independent electral commission, kama hattutaweza hili tukubali kushindwa everyday. Ghana wameweza kufika walipo sasa because of free electral commision otherwise tutakuwa tunaumia na hawa watawala Wasio na sifa ya hata kuitwa VIONGOZI, we need leaders and not rulers.

Rom
 
Hivi John Mnyika amejitangazia hati-miliki ya Ubungo, si aligombea 2005 na kushindwa. Huko Chadema hakuna wanachama wengine wakajaribu kugombea jimbo hili?


Nonsense!

Hujui maana ya hati miliki wewe
 
Kwa hali ilivyo sasa ubungo, hakuna atakayemchagua mbunge toka CCM,Mnyika ana nafasi ya kushinda. Mwangunga asubiri viti maalum.

Kweli kabisa mkuu. Hata 2005 CCM haikushinda kule Ubungo, waliiba kura kumuwezesha Keenja kumshinda Mnyika. Hilo jimbo CCM wahesabu wameshalipoteza. Vyama vingine viungane vichague mzalendo mmoja mwenye mtazamo chanya wamuweke hapo na atapata ushindi wa 'kishindo'!
 
sasa watalipoteza vipi wakati wana uwezo wa kuiba kura?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…