GE2025 Shamsia Mtamba achukua fomu kutetea kiti chake cha ubunge jimbo la Mtwara Vijijini

GE2025 Shamsia Mtamba achukua fomu kutetea kiti chake cha ubunge jimbo la Mtwara Vijijini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Bi Shamsia Aziz Mtamba leo amejitokeza rasmi katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Vijijini kuchukua fomu ya kugombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Bi Shamsia Mtamba ambaye amewahi kulitumikia jimbo hilo kwa miaka tano, amesema ameamua kugombea tena ili kuendelea kuwatumikia wananchi wake na kuendeleza miradi ya maendeleo aliyoianzisha kipindi cha nyuma.

“Naamini bado nina mengi ya kuwafanyia wananchi wa Mtwara Vijijini. Kuna miradi ya elimu, afya, na miundombinu ambayo bado inahitaji kusimamiwa ipasavyo.

Nimerudi tena kuomba ridhaa yao kwa mara nyingine,” amesema Mtamba mara baada ya kuchukua fomu.

SHAMSIA MTAMBA ACHUKUA FOMU KUTETEA KITI CHAKE CHA UBUNGE JIMBO LA MTWARA VIJIJINIAliyekuwa Mbu.jpg
 
Anapitia chama gani? Maana cuf imebakia mfukoni tu
 
Back
Top Bottom