Shangwe Ayo: Viongozi Wakuu wa ACT Wazalendo watafanya ziara kwenye Mikoa 22 na Majimbo 125 Tanzania Bara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT WAZALENDO)

TAARIFA KWA UMMA
VIONGOZI WAKUU WA ACT WAZALENDO KUFANYA ZIARA KWENYE MIKOA 22 TANZANIA BARA
IMG-20240717-WA0028.jpg

Kuanzia tarehe 22 Julai 2024, Viongozi Wakuu wa ACT Wazalendo watafanya ziara kwenye Mikoa 22 na Majimbo 125 Tanzania Bara kwa ajili ya kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utaofanyika mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kama ifuatavyo;-

Kiongozi wa Chama Ndugu Dorothy Semu atatembelea Majimbo 30 kwenye Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Singida na Manyara.

Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Isihaka Mchinjita atatembelea Majimbo 38 kwenye Mikoa ya Ruvuma, Mkoa wa Kichama wa Selous, Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga.
Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu atatembelea Majimbo 21 kwenye Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Geita na Kagera.

Kiongozi wa Chama Mstaafu Ndugu Zitto Kabwe atatembelea Majimbo 36 kwenye Mikoa ya Kigoma, Rukwa, Katavi, Tabora, Mkoa wa Kichama Kahama na Shinyanga.

Pamoja na mambo mengine, kupitia ziara hii, Chama cha ACT Wazalendo kitazindua mpango wa kusajili wanachama wapya Milioni 10 ndani ya Miezi 10 kuanzia Mwezi Julai 2024 na Aprili 2025.

Pia, kwenye ziara hii, viongozi wakuu wa Chama watawahamasisha Watanzania kujiandikisha kuwa wapigakura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025 ili kuhakikisha kuwa Chama kinapata ushindi wa kishindo kwenye chaguzi hizo.

Mbali na hayo, kupitia ziara hii, viongozi wakuu watasikiliza kero mbalimbali za wananchi za kiuchumi, kijamii na kisiasa, kuzipazia sauti na kuendelea kuinadi ahadi ya Chama cha ACT Wazalendo kwa Watanzania ya kujenga Taifa la Wote, Maslahi ya Wote.

Tunawakaribisha Watanzania wote kushiriki ziara hii ili kwa pamoja, tuijenge Tanzania ya Wote, kwa Maslahi ya Wote.
Imetolewa na;

Shangwe Ayo
Naibu Katibu Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
ACT Wazalendo
17 Julai, 2024.
 
Mama kaishatoa fungu la kugharamia hizo posho?
 
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT WAZALENDO)

TAARIFA KWA UMMA
VIONGOZI WAKUU WA ACT WAZALENDO KUFANYA ZIARA KWENYE MIKOA 22 TANZANIA BARA
View attachment 3044945
Kuanzia tarehe 22 Julai 2024, Viongozi Wakuu wa ACT Wazalendo watafanya ziara kwenye Mikoa 22 na Majimbo 125 Tanzania Bara kwa ajili ya kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utaofanyika mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kama ifuatavyo;-

Kiongozi wa Chama Ndugu Dorothy Semu atatembelea Majimbo 30 kwenye Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Singida na Manyara.

Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Isihaka Mchinjita atatembelea Majimbo 38 kwenye Mikoa ya Ruvuma, Mkoa wa Kichama wa Selous, Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga.
Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu atatembelea Majimbo 21 kwenye Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Geita na Kagera.

Kiongozi wa Chama Mstaafu Ndugu Zitto Kabwe atatembelea Majimbo 36 kwenye Mikoa ya Kigoma, Rukwa, Katavi, Tabora, Mkoa wa Kichama Kahama na Shinyanga.

Pamoja na mambo mengine, kupitia ziara hii, Chama cha ACT Wazalendo kitazindua mpango wa kusajili wanachama wapya Milioni 10 ndani ya Miezi 10 kuanzia Mwezi Julai 2024 na Aprili 2025.

Pia, kwenye ziara hii, viongozi wakuu wa Chama watawahamasisha Watanzania kujiandikisha kuwa wapigakura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025 ili kuhakikisha kuwa Chama kinapata ushindi wa kishindo kwenye chaguzi hizo.

Mbali na hayo, kupitia ziara hii, viongozi wakuu watasikiliza kero mbalimbali za wananchi za kiuchumi, kijamii na kisiasa, kuzipazia sauti na kuendelea kuinadi ahadi ya Chama cha ACT Wazalendo kwa Watanzania ya kujenga Taifa la Wote, Maslahi ya Wote.

Tunawakaribisha Watanzania wote kushiriki ziara hii ili kwa pamoja, tuijenge Tanzania ya Wote, kwa Maslahi ya Wote.
Imetolewa na;

Shangwe Ayo
Naibu Katibu Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
ACT Wazalendo
17 Julai, 2024.
Ziara ya kuinanga CHADEMA as if kodi za nchi hii zinakusanywa na CHADEMA.
 
Back
Top Bottom