Shaq awaambia watoto wake watafute mali zao

Shaq awaambia watoto wake watafute mali zao

MIMI NDIO TAJIRI WATOTO WANGU WATAFUTE PESA ZAO

Nyota wa zamani wa #NBA , #ShaquilleRashaunO'Neal amewachana watoto wake sita kuwa Pesa alizonazo na Utajiri alionao sio wao bali ni wa kwake hivyo na wao wajitafutie pesa zao.

Mpaka sasa Shaq anakadiriwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Sh.Trilioni 1 na anaamini kuwa pesa hizo amezitafuta yeye na sio watoto wake kauli yake kwa watoto wake ni "Sisi sio Matajiri, Mimi ni Tajiri" kauli ambayo watoto wake hawapendezwi nayo.
View attachment 2936962
Mablacks ni wabinafsi sana mpaka kwenye familia zao, mbona wazungu wanapesa nyingi na sijawahi skia mzungu awaambie Watoto tafteni Mali zenu hizi sio zenu ni zangu.

Hivi rangi nyeusi huwa Ina matatizo gani
 
Ni vizuri watoto wakijitafuta kivyao, hawezi kuwanyima hata msingi. Hii ya kuwaaminisha watoto kuwa mali ni zao kuna namna inawalemaza kwenye utafutaji, wengi wakishajua baba anazo na ni zao wanabweteka sana. Hasa ngozi nyeusi mwisho wa siku hata wakiachiwa kuzisimamia inakuwa shida.
 
Kama amewapatia Elimu nzuri na kuwasaidia pa kuanzia siyo mbaya, japo kuna Watoto wengine wakishagundua wazazi wana uwezo hawapendi kujishughulisha wanabaki kusubiria mali za kurithi.
 
Shaq sio mjinga hiyo ameongea general, lakini kimsingi najua amewapa elimu nzuri, exposure na kuwawezesha kufanya uwekezaji. Na hili ni jukumu la lazima. Mambo ya mtoto kubweteka kusoma kwa bidii hutaki, kujifunza hutaki, kupambania ndoto zako hutaki ati wasubiri mgao. Hapo hapana.
 
Yuko wapi, maana mimi ndio nimeanza 30 😂
Wale wa kko,magomeni,kinondoni
Utakuta watoto muda wote wanasikilizia mali tu 😄
Ila kuna mzee mmoja alinifurahishaga sana urithi alimpa mtu baking kabisa watoto zake aliwamwaga,maana watoto walikuwa wanamzingua sana

Ova
 
Shaq sio mjinga hiyo ameongea general, lakini kimsingi najua amewapa elimu nzuri, exposure na kuwawezesha kufanya uwekezaji. Na hili ni jukumu la lazima. Mambo ya mtoto kubweteka kusoma kwa bidii hutaki, kujifunza hutaki, kupambania ndoto zako hutaki ati wasubiri mgao. Hapo hapana.
Nanhoyo ndy tatizo kubwa tanzania,baba akiwa na vimali
Kidogo watoro wanabweteka
Wao ni kusikilizia mali tu

Ova
 
Huyu ni MPUMBAVU kwani watoto waliomba kuzaliwa? Starehe zake na hawara yake ndiyo zimeleta mimba na hatimaye watoto unless awarudishe walikotoka
Wewe ndiyo mpumbavu ujue. Kila mtu anatafuta vyake. Mfano mimi niliambiwa hivyo na babu yangu kuwa ukoo wetu hakuna urithi. Hivyo sikupata urithi toka kwa baba, na mimi mtoto yuko tumboni namweleza hivyo. Kwa sasa watoto wangu wana hela kunizidi. Shida inakuwa, sina wa kunisaidia kumanage biashara zangu maana kila mtu anamanage vyake.

Acha utegemezi, kazi ya mzazi ni kukulea kukupatia elimu nzuri hadi hapo unapoona unaweza kujitegemea mnatemana. Hayo ndiyo maendeleo ya familia
 
Huyo mzee ipo siku wanawe watakuja kumfanyia kitu mbayq Sana Wala hataamini.
 
Back
Top Bottom