NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Miaka 10 iliyopita kuna kipindi nilikuwa nimejiandaa kujiua, nilipanga kabisa muda na siku, nilishaandika hadi barua.
Sintosahau 2013 nilivyotaka kujiua nikiwa nimeshamaliza form 4 matokeo yametoka na nimefeli, nyumbani nipo nipo tu kama zigo, wazazi walilalamika kachoma pesa kunisomesha kwa taabu sana kwa kujibana kunisomesha tangu shule ya msingi ya kiingereza hadi shule private secondary.
It was painful, yalikuwa ni maumivu sana kukaa pale nyumbani, basi ili kuanza kutafuta mwanya wa kuchomoka pale nyumbani nikaenda mtaani kujifunza useremala bila ada ila kwa manyanyaso na matusi halafu hata msosi ni wa manati, narudi nyumbani nako mzee anaanza maneno yake "wenzako wanasoma watakuja kuzunguka na viti maofisini huku wewe unahangaika na mambao tu " dah ilikuwa inauma sana yani, nae mama anauliza "unalipwa shilingi ngapi" maksudi kabisa, naanza a e i o yani kigugumizi. hili swali linasugulia chumvi kwenye kidonda maana nilikuwa silipwi chochote hata nauli hakuna.
Nakumbuka mwezi wa kwanza ule katuka ile miezi mitatu ambayo nikiwa bado silipwi chochote huku nafundwa kwa manyanyaso, nyumbani nako mshua na maza wananiona mzigo, nilipatwa msongo mkubwa sana wa mawazo ya kujitoa uhai, niliona maisha haya siyawezi kabisa.
ila ghafla nikiwa nipo lwenye mood ambayo nishaamua liwalo na liwe yani sifikirii chochote zaidi ya kujiua nikaanza kufukiria watu ambao wana changamoto za kiafya ila wanapambana na maisha, watu wanaokuja mjini wanalala kwenye maboksi riziki wanaipata kwa kuuza karanga, watu waliofungwa jela tena kwa makosa ya kubambikiwa, n.k. nikajiona mimi nina afadhali, nilichana chana kile kikaratasi cha ujumbe wa goodbye.
Nilirudi kazini nikiwa na ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya, bidii niliongeza na yale manyanyaso yalipungua kadri nilivyokuwa naanza kujua vitu vingi, nyumbani nako yale maneno nikawa sugu nayapotezea tu maana najua kuna kitu tayari nakifanya ambacho kitakuja kunipa ridhiki na kunifanya nijitegemee,
Kufupisha stori niliweza kuanza kupata vijisenti, kupata elf 5 ikawa kawaida nikawa napeleka hata mboga na matunda nyumbani, mzee akawa anaendelea na mambo yake kwamba wenzanu wanasoma lakini nikawa nimeshajifngua akili kwamba cha muhimu nimepata mlango wa kujitaftia ridhiki yangu.
Nilihama nyumbani nikaenda kupanga ghetto, mitaa ilinifunza nikawa na njaa zaidi ya kujitaftia changu, hadi sasa nilipo nipo na familia yangu, nimepanga nyumba huku naendelea kujenga yangu, n.k.