Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

NBC: nimefungua account , nadhani ni malengo ni kwa muda wa mwaka mmoja!
Ila ku-save kunahitaji nidhamu ya hali ya juu sana, kila pato lango nimeliwekea mgawanyo ufuatao:-
1. 20% ya kila pato langu= Tithe and Offerings
2. 20% = matumizi yote.
3. 30% = Investment
4. 30% = savings i.e investment ya muda mrefu.
Changamoto kubwa ni kupoteza nidhamu hiyo sometime, though najitahidi kujirudi kila mara!
 
Ya ningumu sana kuweka akiba bila kujua lengo LA hiyo pesa...Mfano unahitaji million 7 kwa mwaka lazima uwe na target hii itakusaidia kuwa na Self motivation


Bila kujua lengo lakuweka pesa uwezi kuwa na nidhamu ya ku-save

Unatakiwa uandae Goals kwamba nahitaji nisave ili ninunue mfano Gari or Simu nk...... Njia hii inakusaidia kuongeza Ujasili


Ands of the day kusave pesa inakua ndio sehemu yako ya maisha.....
 
Uko sahihi kabisa!
 
Mshahara wng unapitia NMB! Nikafungua NMB BONUS ACCOUNT! Na kuna form nikajaza kuruhusu kila tarehe 25, Kiasi cha TSHs 615k kihamishwe kwenda Bonus Acc! Uzuri hii Bonus Acc haina ATM Card, Kutoa hela mpk uzame ndani! Binafsi siko interested na Bonus yao.... Shida yng ni ile saving yangu tu!

Changamoto ni kwamba system ya bank lazima ikute hela Ktk account mama ya Mshahara kila tarehe 25, km Siku Mshahara utachelewa zaidi ya tarehe 25 itakuwa ttz!
 
Well said
 
Fedha yako ni ile iliyoko mikononi mwako;ile iliyoko bank n.k inawezekana muda wowote isiwe yako na inaweza kuwa kule na usiipate kwa muda unaotaka,fedha yako mwenyewe inabidi unyenyekee ili kuipata.Nashauri tuwe na utaratibu wa fedha kuingia na kutoka katika biashara zetu....kuliko kupeleka huko kwingineko ndio wazungushe fedha zetu na kujinufaisha.
 
Exactly.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi natumia njia ya kununua hisa VICOBA, kila wiki mwanachama lazima anunue hisa walau moja usipofanya hivyo ni faini.

Njia nzuri sana hii, unajikuta unaweka akiba kwa lazima
Hii naitumia hata mimi kwa week naweka 32000tsh baada ya mwaka mnavunja, hope mwaka huu mwezi wa 8 nitakuwa pazuri ameen.... maana ilianza tangu mwezi wa 8 hadi mwezi wa 8 inakuwa imetimia mwaka, chuo namaliza mwezi wa 6 mwaka huu so baada ya miezi miwil naenda fata changu+ faida na hela ya mchezo ambayo ulianzishwa kwa ajili ya kusaodoa member mwenye shughuli kama ndoa, mahafali n.k niliwaomba niwe wa mwisho hope nitakuwa pazuri na mtaji nishapata.. saving from boom(heslb)...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm pesa yangu ni ndogo sana abt 520k nachukua 270k nasevu kwa kununua pound au dola na inayosalia ndo matumiz japo ni ngumu sana ila najitahid,lakn pia nikipata viposho kila kiasi kinachozidi elfu 80 nasevu,posho isipozidi hicho kiasi natumia kawaida ili kupunguz ukali wa maisha,,
Pia Kuna njia ya kununua vipande vya UTT bado nafuatilia nikijiridhisha ntaitumia hii pia,lengo langu nisave ndani ya miaka 2 Kuna biznec nimei target
 
Izo pound na dola unahifadhi wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hizo Pound na Dolla nakushauri usiwe unahifadhi nyumbani maana hayo mahela huwa yanaenda na series baada ya mda yanakuwa hayatumiki... Unaweza ukawa na dola ya mwaka 2014 ukaenda siku kubadili upewe tzs ukaambiwa hela hiyo haitumiki tena ukawa umekula hasara, either ufungue akaunt ya dola benki ziwe zinakaa benki utakuwa salama... Kajiunge tu UTT Umoja Fund ni bonge moja la njia salama kutunza fedha na kuwekeza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
This is the one am using too.Sio siri tunafanya hiv na wife tangu nalipwa mshahara wa 400k but mpaka leo my quarter acre with house on it , worth not less than 50M
 
Poa mkuu kwan wanabadilisha kila mda gani? Hiyo ya UTT umoja fund nitaufanyia kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…