Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Mshahara wako unaingilia bank hiyo hiyo ?

- Na Je, nikisema niweke miezi 6 inakubalika au ni kuanzia mwaka !
Mshahara naweka bank ya NBC unaweza chukua hela yako baada ya miezi hiyo nimeshawahi fanya pia japo wanasisitiza ndani ya mwaka
 
Mimi natumia njia ya kununua hisa VICOBA, kila wiki mwanachama lazima anunue hisa walau moja usipofanya hivyo ni faini.

Njia nzuri sana hii, unajikuta unaweka akiba kwa lazima
Yaani hii njia nzuri unahifadhi na kukopa bila kutaka..
 
KIBUBU VS BANK VS M-PAWA, Which is the best Saving technique amongst the three ?
Kibubu unakiwekaje ktk kundi hili la uhifadhi wa akiba? Kibubu hutumiwa na watu wasioweza kuzivumilia pesa zao ktk matumizi iwe ya lazima au lah, yani ni jela ya pesa yake dhidi ya akili yake. Huu ni ijinga+
 
Ha ha ha pole sana,njia ni kuamua kwa vitendo na uwe una vipaumbele ambavyo umevioanisha kwamba kinaanza hiki,kinafuata hiki,maana wanapofel weng ni kupanga matumiz kabla hujashika hela yenyewe.. Utakapoipata itaisha tu na utaona haitoshi
Sijui labda nipate elimu kidogo juu ya matumizi ya pesa maana naanza vizur mwaka lakini shida kwenye mwisho wa mwaka najikuta sina akiba ya mwaka mzima.
 
Idea ya mke wangu ya kuweka akiba,ni kunipa nimshikie halafu akianza kuwithdrawal anapitiliza maana mimi Sina slips.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ahaa.Yes naweza kushea kidogo.. iko hivi.. haka kamfumo ni kama ka kununua hisa. mfano mko watu 20, sisi tunafanya hisa moja ni 50,000 na mtu anaweza kununua a maximum of hisa 5 kwa mwezi, that is 250,000. Pia tumeweka kamchango ka jamii shilingi 5,000 kwa kila mwanachama kwa mwezi. Hii inatumika kwa yale mambo ya kijamii yanayotokea mfano kuzaliwa kwa mtoto, harusi, kifo, ugonjwa (japo mtu ana bima ila akilazwa basi angalau wanaomtembelea wanamnunulia chochote)
Kwa hiyo tuna uongozi kwa maana ya myenyekiti, katibu na mweka hazina.. hawa wanahakikisha kila mwanachama amenunua hisa kwa uwezo wake, na pia kila aliekopa anafanya marejesho. na hapo kwenye kukopa ni kwamba unakopeshwa mfano kuanzia milioni moja, marejesho ya riba ni 5% means unalipa 1,050,000 iwe imerudi ndani ya miezi mitatu,..so unaigawanya hiyo kila mwezi unalipa 350,000. Pia mbali na kurejesha lazma pia ununue angalau hisa moja na kuchangia ile gharama ya jamii.. Kwa wanaokopa milioni mbili hadi tatu hiyo marejesho ni miezi sita, na riba yake ni 10%. Huu utaratiu tulijiwekea wenyewe so nyie mkianza yenu mnaweza kujiwekea utaratibu wenu wenyewe. Lengo ni kupata soft loans ambazo zitawasaidia wanachama na si kuwaumiza kama zile za kibenki.
uzuri tunachofanya tuna wahasibu wa hapa kazini nao ni wanachama so wanatunza hesabu yetu vizuri, na pia tunatumia sefu ya ofisini kutunzia fedha yetu kwani hatujafungua account ya chama SILC yetu bado. Kila mwezi wanaandaa excel sheet inayoonesha jumla ya akiba mtu aliyo nayo kwa maana ya hisa alizonunua, madeni, marejesho ya mikopo, deni ambalo mkopaji bado anadaiwa, na ile hesabu ya jamii, na jumla ya fedha yote iliyopo kwenye mfuko toka tumeanza. Kigezo cha kupokea mkopo ni kwamba unakopeshwa mara tatu ya hisa ulizo nazo. mfano kama hisa yako imefika milioni basi una sifa ya kukopeshwa milioni tatu..Na pia kwa kuwa ni watu wa ofisi moja basi kila mwezi baada ya mishahara tu lazma marejesho yafanyike na hisa zinunuliwe..hesabu inafungwa tarehe 30 au 31 ya kila mwezi..mwezi huu wa pili ndo itabidi ifungwe tarehe 28.
Sijui kama kamnofu kamekidhi na kutosheleza, kama kutakuwa na swali jingine i would be glad to share experience tunavyofanya hapa... Karibu
 
Mimi natumia njia hii kusevu akiba. Japo nilichelewa mno mpaka najuta.
Nimepanga kila hela ntakayopata ya marupurupu tofauti na mshahara wangu. Nimekuwa nikiweka kwenye kibubu.
Nina vibubu viwili kimoja cha sarafu na kingine cha noti.cha noti ndo cha marupurupu. Na sarafu ni hela za matumizi ambazo nabakiwa nazo nikirudi Kutoka kwenye majukumu yangu.
Inanisaidi Sana.
 
Asante kwa maelezo mazuri na yalioshiba nimeielewa vizuri sana ingawa hapo kwenye hisa tena ndio changamoto maana sikusoma uchumi so sielewi hisa ni nini, ni fedha au nini?

Jingine pia, sijui sijaelewa vizuri kwamba kwa kila mwezi ni lazima mtu achangie (au anunue hisa) za 250,000 au hyo ni maximum maana umesema hisa moja ni Tshs 50,000/= na kama ni hivyo wakati wa kugawana profit mwisho wa mwaka vipi haiwezi kuleta mkanganyiko wa kugawana faida maana kuna wengine yaweza kua wametoa zaidi ya wenzao?

Na vipi Kuhusu memba akikopa na akashindwa kurudisha mnamchukulia hatua gani? Hii ni kwamba kwa kuwa sisi ni bado wachanga tutakapoanza moja kwa moja tufuate km nyie mnavyofanya hadi hapo ambapo tutakuwa tumekomaa vizuri na kuweka sheria zetu wenyewe

Nimependa jinsi ambavyo mambo yako kwa uwazi kwenye hiyo system yenu maana kama kuna records zinaonesha pesa imeshachangwa shs ngapi, kila member amechanga shs ngapi na nani na nani wamekopa (na ni kiasi gani kila mtu amekopa) na salio lililobaki ni shs ngapi. Hapo nimepiga saluti kwa kweli ni very clear management and transparency mlionayo.

I'm still have a lot to learn from you once again.......
 
ndugu jitahidi uwe unarudia kusoma ulichokiandika kabla hujaposti...
na kama unaamini kuwa watu wanaweka akiba ili watoboe basi ni wewe ndio mwenye mawazo potofu!
 
ndugu jitahidi uwe unarudia kusoma ulichokiandika kabla hujaposti...
na kama unaamini kuwa watu wanaweka akiba ili watoboe basi ni wewe ndio mwenye mawazo potofu!
hajui kama wanaoweka akiba wenye kujitambua wanakusanya mtaji wa kufanya jambo kubwa ili ndo wafikie hayo malengo ya kutoboa na sio kama anavyojadili yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…