Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Tumeanzisha mfumo wa SILC( Saving and Internal Lending Community) ofisini..naweza kuweka hadi 250,000 kwa mwezi.. Pia mwanachama anaweza kupata mkopo na kurudisha kwa riba ambayo ni 5-10% kulingana na kiasi anachochukua na muda..Uzuri ni kwamba wote ni wafanyakazi hapa na ukishasave hela yako huna mwisho wa mwaka tunafanya share out, unapata hela yako yote uliyosave na ile riba iliyopatikana inagawanywa..Ingekuwa kibubu maana yake ile unayoweka ni hiyo hiyo haiongezeki
Hiyo mbona ni SACCOS aka VICOBA
 
Hongera hujawahi kutana na changamoto zozote zile ?
changamoto ni muda mrefu wa kukusanya vifaa ila sijawahi kudhulumiwa maana kuweka hela kwa muuzaji ni sawa na kumkopesha mtaji. Kuna jamaa mmoja wa matofali aliwahi kunicheleweshea kazi kama kipindi cha mwezi mmoja ila baadae alinipatia. Cha kufanya ni kudeal na watu waaminifu na wenye mitaji mikubwa. Nilikuja kugundua kuwa watu wengi wanafanya hivyo na pia kuwe na rekodi nzuri. Hapa nilipo nina risiti ya tofali 2500 mfukoni nishalipa bado ku-deliver tu nakusanya hela ya materials zingine
 
Hii imekaa vizuri
 
Daaah hapa kwenye kusave mwenzenu nimeshindwa maana kila nikijaribu kusave nakuwa na uhitaji wa pesa nyingi zaidi ya iliyopo sijui nitumie njia gani kwa hili maana natamani sana kuweka akiba but matatizo yananiharibia
 
Mimi nanunua dhahabu kwa sonara na kuihifadhi na zingine wife na watoto wanazivaa wakihitaji
Ni asset nzuri na thamani haishuki hata siku moja
Unaweza kupeleka bank kama kuna access hiyo kwa huko
Zikipotea je?
 
mie nina mbinu ambayo naitumia katika kazi kama za ujenzi ambayo uwa sifanyi saving kama hizi mlizozizoea za kuweka fedha kwenye kibubu au mpesa. Nachofanya ni kuandaa ramani na kisha makadirio ya ujenzi (BoQs) kisha nongea na wauza vifaa nakuwa napeleka fedha kidogo kidogo zikikamilika nachukua vifaa kuanzia msumari, nondo mpk cement uwa nafanya hivi. Kwa kweli imenisaidia mpaka sasa nimekuwa kimasamaki Fulani hivi nyumba Zaidi ya nne
Nmependa wazo lako...
 
Mimi napata 250,000 kwa mwezi. Mwanzoni nilikuwa natumia kwanza afu ikibak ndo nasave unakuta mda mwngne hamna hela ya maana uliyosave. Nikabadilisha njia. Nikawa nikipata tu hela naweka 100,000 kamili bank alaf hyo 150 inayobak ndo nafanya matumizi. Namshukuru MUNGU na kipato changu kidg nimekaa mwaka na zaidi sasa nina akiba ya 1.2m
Hyo ndo njia ninayoitumia na sitoiacha. Naombea niongeze kipato ili kuongeza akiba yangu.
Nmekupenda bure aisee.

"SPEND WHAT LEFT AFTER SAVE"
 
Mimi napata 250,000 kwa mwezi. Mwanzoni nilikuwa natumia kwanza afu ikibak ndo nasave unakuta mda mwngne hamna hela ya maana uliyosave. Nikabadilisha njia. Nikawa nikipata tu hela naweka 100,000 kamili bank alaf hyo 150 inayobak ndo nafanya matumizi. Namshukuru MUNGU na kipato changu kidg nimekaa mwaka na zaidi sasa nina akiba ya 1.2m
Hyo ndo njia ninayoitumia na sitoiacha. Naombea niongeze kipato ili kuongeza akiba yangu.
Njoo pm tuyajenge
 
Hongera mkuu kwa uthubutu huo wa kuweka elf 30 per day si kitu kidogo katika hali hii ya vyuma kukaza

(30,000 x 365= 10,950,000 x 5 = 54,750,000)

Je unakumbana na changamoto zipi?
Huenda lakini.........! Elfu 30 kwa siku ni biashara ya uhakika tena isiyokuwa na changamoto
 
Kwa kuongea eti itafika 150m ni rahisi kishenzi,ingia kwenye utekelezaji ndo utaona mziki wake.

SMARTNESS ID OVERATED.
ni kweli kuzalisha pesa si kazi rahisi mkuu wakati mwingine unaweza ukapoteza kabisa
 
Huenda lakini.........! Elfu 30 kwa siku ni biashara ya uhakika tena isiyokuwa na changamoto
Ya kawaida tu,maana ili uweze kusave 30k bas upate mada tatu yake per day,ambayo ni kawaida tu kama unafanya biashara yenye kueleweka..
 
Daaah hapa kwenye kusave mwenzenu nimeshindwa maana kila nikijaribu kusave nakuwa na uhitaji wa pesa nyingi zaidi ya iliyopo sijui nitumie njia gani kwa hili maana natamani sana kuweka akiba but matatizo yananiharibia
Ha ha ha pole sana,njia ni kuamua kwa vitendo na uwe una vipaumbele ambavyo umevioanisha kwamba kinaanza hiki,kinafuata hiki,maana wanapofel weng ni kupanga matumiz kabla hujashika hela yenyewe.. Utakapoipata itaisha tu na utaona haitoshi
 
Back
Top Bottom