Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Unaweka akiba yako Bank au kwenye kibubu
 
Nitaijaribu hii mana nilikua naweka sarafu kwene mkoba mbona ilinishinda
Nilikuwa naweka sarafu za 500, kwa bidii sana, baada ya mwezi wife akawa anachukua na kufanyia matumizi madogo madogo, maana niliweka kwenye mkoba wake asioutumia. Baadaye nikaghairi na nikaishia kutoa elfu 50 tu!
 
Kibubu unakiwekaje ktk kundi hili la uhifadhi wa akiba? Kibubu hutumiwa na watu wasioweza kuzivumilia pesa zao ktk matumizi iwe ya lazima au lah, yani ni jela ya pesa yake dhidi ya akili yake. Huu ni ijinga+
Acha wenge
 
Unaishi wapi....
Kazini kwako unatumia usafiri gani kufika?
Napata shida kidogo kuona uhalisia ktk hoja yako mkuu, japo ni nzuri kinadharia
 
Unaishi wapi....
Kazini kwako unatumia usafiri gani kufika?
Napata shida kidogo kuona uhalisia ktk hoja yako mkuu, japo ni nzuri kinadharia
Uhalisia upo kwasababu sina majukumu mengi.
Kazini na nyumban napanda daladala moja kwaivyo ni 800 kwenda na kurudi.
Chakula napata kazini.
Kwaivyo matumizi yangu ni hyo 800 ya usafiri alafu nakaa kwetu.
Ila pia kazini na nyumban sio mbal mda mwngne natembea tu mdg mdg hadi nafika.
Uhalisia upo tofauti ni majukumu tu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mimi natumia vibubu ninavyo 2 kimoja nahifadhi coin (500 ) kila siku nikirudi home najisachi nikikuta 500 natumbukiza kibubu kimekaribia kujaa kibubu cha pili nahifadhi noti (500,au 10000) ambazo ninazipata kwenye investment zangu.Pia nina application kwenye simu ambayo narekodi Expense na Income zangu kila siku (Daily Expenses,Spending Tracker)
Baadae nitazibadilisha kwenye $ niweke kwenye account
 
Ok, hapo nimekupata mkuu..
Bila shaka upo Mwanza kama mimi...
 
Mkuu naungana na wewe lakini pia kumbuka watu wana save kwa malengo tofauti. Mfano kama mtu ameajiriwa ila analengo la kufungua duka la 5m, lakini salary yake ni 400k. Huoni kama anatakiwa kusave hadi apate hiyo 5m ili afungue duka? Maana wengine kwa nature ya ajira zao hata benki hawamkopeshi hiyo hela anayotaka. Au kuna alternative yoyote?

Mawazo yako mkuu
 
Hii mzuri, japo kwa sisi ndugu zenu (waislamu) hatutakiwi kufanya biashara ya riba. Lakini nimependa mawazo yako tangu umeanza kuchangia. Na naamini hata katika mfumo huo wa bila kuweka riba tunaweza na sisi kufanya umoja huu japo mtaji hautokuwa kwa kasi kama nyie
 
Ofisini kwetu tuna vicoba kama hiyo huu mwaka wa nne ila kwetu hatuweki ribs ukikopa milioni unalipa hiyo hiyo sema Katibu ni mnoko hajui shida ni utalipa tu na tunafanikiwa.
 
kweli baba, mnaamua tu namna ambavyo mnaweza kufanya iendane na matakwa yenu ya kiuchumi bila kukwaza imani zenu pia.. sisi tunafanya hivyo kwa kuwa kiimani haina shida kwa wanachama waliopo.. goodluck
 
Nasave kwa kucheza michezo na vicoba. Umenikumbusha nimeanza kusave primary kwenye kibubu mimi na ndugu yangu tulikua tunaweka 200 kila siku. Tuliweka kama miezi mitatu kwenye kibubu chetu kipya. Kuja kukifungua tukakuta elfu 2. Sitasahau machungu yake. Kuna dada yetu alikifungua akaiba hela halafu akakifunga kama kilivyo.
 
Lahaulaaa lakwata.....[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
Kumbe una dadaako mkora....[emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…