Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Lahaulaaa lakwata.....[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
Kumbe una dadaako mkora....[emoji13] [emoji13] [emoji13]
Huyo dadangu/ndugu alishindikana. Katuibia sana hela. Alikua na tabiq za ajabu sana mmbea mgombanishi mwizi na kila kitu.
 
Huyo dadangu/ndugu alishindikana. Katuibia sana hela. Alikua na tabiq za ajabu sana mmbea mgombanishi mwizi na kila kitu.
Pole sana mkuu, kwakua ilikua ni utoto najua atakua alisha badilika
 
Pole sana mkuu, kwakua ilikua ni utoto najua atakua alisha badilika
Asante mkuu. Tabia ya wizi hajaacha bado. Alikuw mgombanishi kiasi ambacho alisababishq babu na bibi wakaachana kwa sababu yake. Nimeishi nae kama miaka 15 ila sijawahi kumpenda sasa hivu hata mawasiliano nae sinq kama vile mtu ambae sijawahi kumjua.
 
Ahaa.Yes naweza kushea kidogo.. iko hivi.. haka kamfumo ni kama ka kununua hisa. mfano mko watu 20, sisi tunafanya hisa moja ni 50,000 na mtu anaweza kununua a maximum of hisa 5 kwa mwezi, that is 250,000. Pia tumeweka kamchango ka jamii shilingi 5,000 kwa kila mwanachama kwa mwezi. Hii inatumika kwa yale mambo ya kijamii yanayotokea mfano kuzaliwa kwa mtoto, harusi, kifo, ugonjwa (japo mtu ana bima ila akilazwa basi angalau wanaomtembelea wanamnunulia chochote)
Kwa hiyo tuna uongozi kwa maana ya myenyekiti, katibu na mweka hazina.. hawa wanahakikisha kila mwanachama amenunua hisa kwa uwezo wake, na pia kila aliekopa anafanya marejesho. na hapo kwenye kukopa ni kwamba unakopeshwa mfano kuanzia milioni moja, marejesho ya riba ni 5% means unalipa 1,050,000 iwe imerudi ndani ya miezi mitatu,..so unaigawanya hiyo kila mwezi unalipa 350,000. Pia mbali na kurejesha lazma pia ununue angalau hisa moja na kuchangia ile gharama ya jamii.. Kwa wanaokopa milioni mbili hadi tatu hiyo marejesho ni miezi sita, na riba yake ni 10%. Huu utaratiu tulijiwekea wenyewe so nyie mkianza yenu mnaweza kujiwekea utaratibu wenu wenyewe. Lengo ni kupata soft loans ambazo zitawasaidia wanachama na si kuwaumiza kama zile za kibenki.
uzuri tunachofanya tuna wahasibu wa hapa kazini nao ni wanachama so wanatunza hesabu yetu vizuri, na pia tunatumia sefu ya ofisini kutunzia fedha yetu kwani hatujafungua account ya chama SILC yetu bado. Kila mwezi wanaandaa excel sheet inayoonesha jumla ya akiba mtu aliyo nayo kwa maana ya hisa alizonunua, madeni, marejesho ya mikopo, deni ambalo mkopaji bado anadaiwa, na ile hesabu ya jamii, na jumla ya fedha yote iliyopo kwenye mfuko toka tumeanza. Kigezo cha kupokea mkopo ni kwamba unakopeshwa mara tatu ya hisa ulizo nazo. mfano kama hisa yako imefika milioni basi una sifa ya kukopeshwa milioni tatu..Na pia kwa kuwa ni watu wa ofisi moja basi kila mwezi baada ya mishahara tu lazma marejesho yafanyike na hisa zinunuliwe..hesabu inafungwa tarehe 30 au 31 ya kila mwezi..mwezi huu wa pili ndo itabidi ifungwe tarehe 28.
Sijui kama kamnofu kamekidhi na kutosheleza, kama kutakuwa na swali jingine i would be glad to share experience tunavyofanya hapa... Karibu
Kama kikundi chetu,.na kuongezea hiyo riba inagawanywa kwa wanachama mwisho wa mwaka !!
 
Mi mshahara ukishaingia nitatoa nitakachotoa lkn kuna limit ikifika sitoi ng'o!
 
Mkuu kibubu sitakaa nirudie! Kulikuwa na kibubu kinatolewa na NMB miaka ya nyuma. Kila siku nikawa naweka hela yoyote inayobaki kwenye matumizi ya siku na nikafanya kwa uaminifu kwa muda wa mwaka mzima. Siku moja nikakihamisha halafu nikasahau nilipokiweka, wee nusura nizimie! Sasa hivi jukumu hilo nimemwachia mama watoto amefungua akaunti ya malengo. Huko kila siku anapeleka elfu 30 kutoka kwenye Biashara! Hii ni njia salama kabisa!
Kibubu cha NMB ukakihamisha? Una maana gani mkuu?
 
Mi mshahara ukishaingia nitatoa nitakachotoa lkn kuna limit ikifika sitoi ng'o!
Una moyo aisee
Mie siwezi kukaa na hela
Yaani nimeshindikana,VICOBA + michezo + shemeji ni kimbilio langu.
 
Mimi naweka malengo account ya NBC Kila mwezi nakatwa direct kutoka kwenye mshahara kwa mwaka mzima imenisaidia sana.njia ya vibubu ilinishinda nilikua navunja kabla sijafikisha malengo.
Hii nayo ni nzuri.
 
Nasave kwa kucheza michezo na vicoba. Umenikumbusha nimeanza kusave primary kwenye kibubu mimi na ndugu yangu tulikua tunaweka 200 kila siku. Tuliweka kama miezi mitatu kwenye kibubu chetu kipya. Kuja kukifungua tukakuta elfu 2. Sitasahau machungu yake. Kuna dada yetu alikifungua akaiba hela halafu akakifunga kama kilivyo.
😀😀😀
poleni sana kwa yaliyo wakuta
 
Mkuu kibubu sitakaa nirudie! Kulikuwa na kibubu kinatolewa na NMB miaka ya nyuma. Kila siku nikawa naweka hela yoyote inayobaki kwenye matumizi ya siku na nikafanya kwa uaminifu kwa muda wa mwaka mzima. Siku moja nikakihamisha halafu nikasahau nilipokiweka, wee nusura nizimie! Sasa hivi jukumu hilo nimemwachia mama watoto amefungua akaunti ya malengo. Huko kila siku anapeleka elfu 30 kutoka kwenye Biashara! Hii ni njia salama kabisa!
Sio unafanya promo mkuu
 
Back
Top Bottom