Ahaa.Yes naweza kushea kidogo.. iko hivi.. haka kamfumo ni kama ka kununua hisa. mfano mko watu 20, sisi tunafanya hisa moja ni 50,000 na mtu anaweza kununua a maximum of hisa 5 kwa mwezi, that is 250,000. Pia tumeweka kamchango ka jamii shilingi 5,000 kwa kila mwanachama kwa mwezi. Hii inatumika kwa yale mambo ya kijamii yanayotokea mfano kuzaliwa kwa mtoto, harusi, kifo, ugonjwa (japo mtu ana bima ila akilazwa basi angalau wanaomtembelea wanamnunulia chochote)
Kwa hiyo tuna uongozi kwa maana ya myenyekiti, katibu na mweka hazina.. hawa wanahakikisha kila mwanachama amenunua hisa kwa uwezo wake, na pia kila aliekopa anafanya marejesho. na hapo kwenye kukopa ni kwamba unakopeshwa mfano kuanzia milioni moja, marejesho ya riba ni 5% means unalipa 1,050,000 iwe imerudi ndani ya miezi mitatu,..so unaigawanya hiyo kila mwezi unalipa 350,000. Pia mbali na kurejesha lazma pia ununue angalau hisa moja na kuchangia ile gharama ya jamii.. Kwa wanaokopa milioni mbili hadi tatu hiyo marejesho ni miezi sita, na riba yake ni 10%. Huu utaratiu tulijiwekea wenyewe so nyie mkianza yenu mnaweza kujiwekea utaratibu wenu wenyewe. Lengo ni kupata soft loans ambazo zitawasaidia wanachama na si kuwaumiza kama zile za kibenki.
uzuri tunachofanya tuna wahasibu wa hapa kazini nao ni wanachama so wanatunza hesabu yetu vizuri, na pia tunatumia sefu ya ofisini kutunzia fedha yetu kwani hatujafungua account ya chama SILC yetu bado. Kila mwezi wanaandaa excel sheet inayoonesha jumla ya akiba mtu aliyo nayo kwa maana ya hisa alizonunua, madeni, marejesho ya mikopo, deni ambalo mkopaji bado anadaiwa, na ile hesabu ya jamii, na jumla ya fedha yote iliyopo kwenye mfuko toka tumeanza. Kigezo cha kupokea mkopo ni kwamba unakopeshwa mara tatu ya hisa ulizo nazo. mfano kama hisa yako imefika milioni basi una sifa ya kukopeshwa milioni tatu..Na pia kwa kuwa ni watu wa ofisi moja basi kila mwezi baada ya mishahara tu lazma marejesho yafanyike na hisa zinunuliwe..hesabu inafungwa tarehe 30 au 31 ya kila mwezi..mwezi huu wa pili ndo itabidi ifungwe tarehe 28.
Sijui kama kamnofu kamekidhi na kutosheleza, kama kutakuwa na swali jingine i would be glad to share experience tunavyofanya hapa... Karibu