Asante mkuu. Nitalitembelea kuchekiBei inategemea na aina mfano whey protein hua naona zinaanzia 60k, 80k, 120k, na kuendelea.
Na kwa k/koo kuna duka lilikua pale Shimoni
Nakubaliana na wewe ndugu Mwenyekiti..Kitu poa kabisa baada ya kuanza mazoezi ni kupata matokeo ya zoezi lako, poa zaidi ni matokeo hayo yanapokuja kwa haraka.
Siyo kila mtu ana muda wa kufanya zoezi la masaa matatu, hell wengine hata saa moja kwao ni kupoteza muda.
Now uzi huu uwe special kwa ajili ya kugeana mbinu za kufikia malengo haraka, mbinu zitakazotolewa hapa ni za mazoezi yoyote.
Ni vizuri mbinu itakayotolewa iwe ambayo mtu ulishawahi kuitumia au kuiona mtu akiitumia ili likija swali unalijibu kwa uhakika.
Naanza na hizi.
1. Ukiwa unajivuta mikono usiitanue sana iwe na umbali wa usawa wa mabega yako.
Utatengeneza biceps, nguvu za mikono, mabega na 'mabawa' yatakuja kama kawaida.
2. Raundi zako ziwe 10 na seti 3 za mazoezi katika kila zoezi lako.
3. Kama unafanya zoezi la kifua anza na push ups, piga push ups za tambarare na miguu ikiwa juu ya kitu kisha nenda anza na incline bench press.
4. Ukiwa unakimbia usiteme mate na hema kwa kutumia pua, mdomo usiwe wazi. Utafikia levo ya juu kabisa ya kukimbia kwako pia utazuia kichomi.
5. Tafuta mwenza wa mazoezi.
6. Changanya juisi na peanut butter na itumie muda wote utakaokua ukifanya zoezi lako.
Zingine endeleeni wadau na mimi nitaendelea kutoa mbinu.
Seti malengo ya unachotaka kukifikia kabla ya kuanza tizi.Sina partner wa mazoezi, akitokea huwa wanakuwa wavivu na kupotea ndani ya muda mfupi, napenda mazoezi lakini baada ya muda mfupi napata uvivu na kuacha, naomba mbinu nikianza zoezi nisiache kamwe
Sent from my GT-N5100 using JamiiForums mobile app
Ahsante sana sana mkuu, ngoja niipitieSeti malengo ya unachotaka kukifikia kabla ya kuanza tizi.
Fuata hii routine pia
Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym
Sasa mkuu nisaidie programme, nataka kufanya mazoezi kwa nia mbili kuu;Seti malengo ya unachotaka kukifikia kabla ya kuanza tizi.
Fuata hii routine pia
Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym
Kwenye kupungua napendekeza kukimbia kuwe kila siku, squats, na mazoezi ya tumboSasa mkuu nisaidie programme, nataka kufanya mazoezi kwa nia mbili kuu;
kwanza, nipunguze uzito na unene wa mafuta na kitambi japo si kikubwa.
Pili, nataka kujenga mwili mkakamavu mkono, wing na kifua.
Mazoezi haya yote nataka kufanyia nyumbani.
Mwanzo mgumu je programme ziweje ili niweze ku master zoezi zote utakazo nitajia, Ahsante sana.
Ahsante sana, mkuu naanza rasmi, ili kupata matokeo ya haraka inaweza chukua muda gani?Kwenye kupungua napendekeza kukimbia kuwe kila siku, squats, na mazoezi ya tumbo
Unataka Tumbo Flat na Six Packs? Cheki Hapa
Kwenye wings, kama unaishi nyumba yenye geti unaweza ukatumia lile eneo linaloachwa baada ya kufungua geti kwa ajili ya kujivuta.
Na unaweza ukapiga push ups ukiwa umetanua mikono zaidi ya kawaida.
Katika kuupata mwili mkakamavu, mikono na kifua fuata ile routine ya kwanza kukutumia.
Kama unafuata kila nilichoandika hapo na unakula chakula ipasavyo, unakunywa maji na kupumzika inavyotakiwa.Ahsante sana, mkuu naanza rasmi, ili kupata matokeo ya haraka inaweza chukua muda gani?
Aisee, mkuu ubarikiwe sana upo full detailed nitakufollow kama nitakuwa na maswali zaidi, Usichoke mkuu wangu leo jioni naanza kukimbia rasmi. Nataka jioni niwe nakimbia na kufanya zoezi la tumbo then ahsubuhi nafanya workout za kujenga mkono na kifua. Je natakiwa kupumzika siku yoyote au ni mfululizo kwa week sita. ?Kama unafuata kila nilichoandika hapo na unakula chakula ipasavyo, unakunywa maji na kupumzika inavyotakiwa.
Wiki sita utakua umepata unachotaka.
Hiyo routine ya kukupa kifua, mikono na ukakamavu ndani ya siku tatu utakua ushajiona jinsi ulivyobadilika
Hii ni kwa ajili ya squats
JIFUNZE: Tengeneza Mwili wa chini bila kuingia Gym
Usijioverload chief fanya kidogo kidogoAisee, mkuu ubarikiwe sana upo full detailed nitakufollow kama nitakuwa na maswali zaidi, Usichoke mkuu wangu leo jioni naanza kukimbia rasmi. Nataka jioni niwe nakimbia na kufanya zoezi la tumbo then ahsubuhi nafanya workout za kujenga mkono na kifua. Je natakiwa kupumzika siku yoyote au ni mfululizo kwa week sita. ?
Mkuu hiyo sits up ndio zoezi gani?Ili kuepuka kupoteza muda na kushindwa kufanya baadhi ya mazoezi. Yaunge mazoezi yako katika routine ya siku moja.
Mfano, utapiga push ups 20, ukimaliza utafanya sit ups 20, ukimaliza utapiga squats 20.
Unaanza tena mwanzo na hii iwe bila kupumzika, kwakua hayo mazoezi hayahusiani hivyo hayatagusa eneo moja mara nyingi.
Ni zoezi la tumboMkuu hiyo sits up ndio zoezi gani?