Kitu poa kabisa baada ya kuanza mazoezi ni kupata matokeo ya zoezi lako, poa zaidi ni matokeo hayo yanapokuja kwa haraka.
Siyo kila mtu ana muda wa kufanya zoezi la masaa matatu, hell wengine hata saa moja kwao ni kupoteza muda.
Now uzi huu uwe special kwa ajili ya kugeana mbinu za kufikia malengo haraka, mbinu zitakazotolewa hapa ni za mazoezi yoyote.
Ni vizuri mbinu itakayotolewa iwe ambayo mtu ulishawahi kuitumia au kuiona mtu akiitumia ili likija swali unalijibu kwa uhakika.
Naanza na hizi.
1. Ukiwa unajivuta mikono usiitanue sana iwe na umbali wa usawa wa mabega yako.
Utatengeneza biceps, nguvu za mikono, mabega na 'mabawa' yatakuja kama kawaida.
2. Raundi zako ziwe 10 na seti 3 za mazoezi katika kila zoezi lako.
3. Kama unafanya zoezi la kifua anza na push ups, piga push ups za tambarare na miguu ikiwa juu ya kitu kisha nenda anza na incline bench press.
4. Ukiwa unakimbia usiteme mate na hema kwa kutumia pua, mdomo usiwe wazi. Utafikia levo ya juu kabisa ya kukimbia kwako pia utazuia kichomi.
5. Tafuta mwenza wa mazoezi.
6. Changanya juisi na peanut butter na itumie muda wote utakaokua ukifanya zoezi lako.
Zingine endeleeni wadau na mimi nitaendelea kutoa mbinu.