Share Nasi Hapa Cheat Code Ya Mazoezi Yoyote

Tafadhali usiniquote na kuniuliza juu ya hii mada
 
Mkuu samahani, hapa mrejesho yaani faida ni zipi na baada ya muda gani? Je kwa bigginers waanze na utaratibu upi kwa aina hii ya zoezi? ?msaada please
 
Mimi nilianza zoezi kwa week tatu la squat za kawaida 75, Seti 3 kila moja raundi 25, halafu push up 60 Seti 4 kila moja raundi 15, nilianza taratibu kisha maximum ndiyo nilifikia hapo, ila hiyo week ya tatu niliumwa sana mgongo, na mwili mzima kama homage, ilishindikana kabisa kuendelea nimepumzika kama week sasa, nataka kuanza tena, je wapi nilikosea? ? Ushauri mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika mazoezi maumivu hua hayaji ghafla huanza polepole kisha ukiyapuuzia ndiyo huongezeka.

Squats huleta maumivu kama unatumia mzigo mkubwa au unakaa mkao ambao unasababisha presha kubwa iwe kwenye mgongo. Au kwenda idadi ambazo kwako siyo poa.

Mimi nashauri angalia mkao wako kama unaendana na zoezi linavyotaka, hii inaenda mpaka kwenye push ups jinsi unavyopiga na unavyokaa ili kuzipiga.
 
Mkuu samahani, hapa mrejesho yaani faida ni zipi na baada ya muda gani? Je kwa bigginers waanze na utaratibu upi kwa aina hii ya zoezi? ?msaada please
Push ups za hivi misuli ya msingi itakayoguswa ni ya kifua, secondary muscles ni mabega, triceps na mgongo.

Fanya siku tatu mfululizo kisha ona utakavyojisikia.

Beginner apunguze idadi ya reps na aongeze muda wa kupumzika.
 
Ukisema watu wanaopenda mazoezi basi hata mimi naweza kujiweka napenda sana mazoezi.. Shida yangu ni moja tu nina tatizo la ugonjwa fulani unaitwa chembe ya moyo na nina vidonda tumbo.

Basi nikianza zoezi tu hasa haya ya tumbo siku 2 tu naacha mwenyewe kwani maumivu ya chembe ya moyo yanakuja kwa kasi saana.

Wakati mwingine nakimbilia hili zoezi la kukimbia ambapo inanilazimu nivae nguo nyingi sana nisipigwe baridi kwani baridi ikinipiga tu saana na huku mbeya kulivo baridi baasi kesho siamki nashikwa balaa na maumivu ya chembe ya moyo.

Natamani sana siku nipate tiba ya haya magonjwa mawili nazani ntakuja kuwa na ratiba nzuri sana ya mazoezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba nielekeze mazoez mazuri ya kupunguza mikono na nyama za mgongo(bra straps kwa kina dada)
 
Mkuu naomba nielekeze mazoez mazuri ya kupunguza mikono na nyama za mgongo(bra straps kwa kina dada)
Kuongezeka kwa mafuta na kuizidi misuli ndiyo hupelekea sehemu kuongezeka mpaka kuning'inia.
Mimi napendekeza ufanye aerobics, ukimbie, uruke kamba, punguza vyakula vya mafuta, kunywa sana maji.

Hizo nyama za mgongo haujasema ni kwa chini au juu, kama ni kwa chini mazoezi ya kupunguza tumbo pamoja na hayo juu yanatosha kumaliza hiki kitu.
Kama ni kwa juu mazoezi ya kupunguza fat pekee yanatosha.

Kwenye mikono, kwa kawaida kwa baadhi ya watu wakipunguza nyama za mikono kinachofuata ni nyama kuning'inia suluhisho hapa ni kupiga mpaka push ups.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…