Share za ACACIA zazidi kuporomoka baada ya TRA kupeleka Tax Invoice

Poor thinking yani umpelekee madai hisa zishuke wewe uogope ni zaidi ya woga wa kike.
Na hapo hata mgoni hatujaufunga bado.
Wao wametuongopea wewe ukaa na fikra finyu kiais hicho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwe unasoma vitu uelewa b4 hujachangia hayo ni malimbikizo ya miaka 17 pamoja na penalties zake.
Na sio mwaka mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi tutakuja kupata mwekezaji wa level ya Barrick tena kweli?
Ni heri asipatikane kama ni mwizi, kabla ya Barick miaka ya 1994 wachimbaji wadogo waliingiza kipato kikubwa kuliko hao tuliowaita wawekezaji, Mh Mrema aliwaruhusu wauze madeni kupitia mabenki na hasa NBC, mawazo yangu ni TUNAWATAMANI WAWEKEZAJI LAKINI KAMA NI WEZI MADINI YAACHWE, KIKIJA KIZAZI CHENYE AKILI WATACHIMBA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Dar zipo Mkuu,kuna wazawa wenzio waumia

Pole sana wazawa wenye hisa za ACACIA. Lakini kwa wengine ACACIA ni kampuni la kibeberu, acha hisa zao ziporomoke, kampuni lifilisike, lifungwe, lidaiwe, life. Kama alivyosema Magufuli akiwa Singida leo, ACACIA wakafie mbele!

By the way, wanavyosema ACACIA inachangia pato la taifa, hivi najiuliza, unachangiaje GDP kama mapato yako yote yanapelekwa nje ya nchi? Tena sio yanapelekwa nje, ni kwamba yanabaki nje. Ndege inatua mgodini inachukua dhahabu, malipo yanakuwa yashafanywa.

Tume ya Osoro imesema, na ACACIA wamekiri, kwamba makontena ya makinikia yanakuwa yashalipiwa na wateja huko huko Ulaya kabla hayajaondoka nchini, hivyo mteja yuko Ulaya; wana hisa wako London; benki ya ACACIA iko London. Pesa huku inakuja kufanya nini? Haikanyagi. Inaingiaje kwenye hesabu za GDP ya Tanzania?
 
Inaingia kwenye GNP

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app
 
Inaingia kwenye GNP

Same difference.

Take one divide by the population you get the other.

Pesa ambayo imelipwa na mteja New York kwenda benki ya ACACIA London, wakalipwa wanahisa London, haijagusa mzunguko wa pesa Tanzania, inaingia vipi kwenye GNP ya Tanzania?
 
Ombeni madai yenu yawe ya kweli vinginevyo tutawafidia hiyo hasara.

Cha ajabu hata ripoti hamtaki kuwapa sasa sijui tutaaminika vipi..
Mchanga si wanachimba wao !? Watayarishe ripoti yao wenyewe
 
Wakati ripoti zinatayarishwa, kuna watu walidukuliwa simu zao na kufuatiliwa nyendo zao wakati wakiifuatilia tume zote mbili
 
Wao wanadai miaka yote wamechimba kwa hasara, tunawasaidia wasiendelee kupata hasara !
 
Ni shida yao, wajipange kupambana nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Humu jf kuna vijitu vijinga sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu data nyingi za wazungu ziko wazi ukizitafuta utapata sasa hapa kwetu ripoti tumeambiwa ni ya rais!! hata anayetuhumiwa hajapewa huu si ujinga wa kiwango cha lami aka uzazwa!
Ripoti za acacia wanadai wanapata hasara miaka yote waliokuwepo hapa katika migodi yote ! Au hukumsikia CAG !?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…