Shariff Abdallah Attas: Rafiki wa Nyerere aliyemsahau


Kama waliweza kukutana physically halafu bado hakuweza kumtambua, nafikiri alikuwa analake jambo..
 
Bora Mimi rafiki yangu Nyambelele bado tunakumbukana tokea tukiwa watoto mpaka sasa tumekuwa wahenga,kujifanya umemsahau mtu ni hulka ya mtu tu wala siyo kwamba eti unakuwa umezungukwa na usalama.
kusahau kupo hasa ukiwa na majukumu mengi Mzee Attas alitakiwa kumukumbusha Nyerere kuwa yeye ni Attas waliokuwa wanakatisha mitaa pamoja kufuata ugali kwa Abdulwahid miaka ya kabla ya uhuru,mwenyekosa hapo ni Attas mwenyewe.
 
Tatizo la waswahili, kwani kulikuwa na tatizo kama angejitambulisha???? Mambo mengi kwa viongozi wetu
 
Marehemu aendelee kusubiri?!

Sasa ni nani huyo anayeleta hizi habari kwamba alisahauliwa? Kumbe mtu mwenyewe alishatangulia mbele za haki na huenda ameshapokea malipo yake yasiyo na upendeleo.
 
Sasa ni nani huyo anayeleta hizi habari kwamba alisahauliwa? Kumbe mtu mwenyewe alishatangulia mbele za haki na huenda ameshapokea malipo yake yasiyo na upendeleo.
Jamaa angepotezea tu hii mada maana wahusika wote washatangulia mbele ya haki.
 
Mimi nafikiri Mzee Attas was too proud of himself, akaona kujitambulisha ataonekana anajikomba au kitu kama hicho. Kwa maelezo hayo aliyotoa inaonekana aliumia sana, hata mimi kwa nafasi yake nimeumia pia. Yalishawahi kunikuta japo naweza kusema ya kwangu yalikuwa madogo tu. Nilipokuwa shule nilikuwa prefect, na kuna bwana wadogo ambao kwa mtazamo wangu wa wakati ule nilikuwa nawalea na waliniheshimu sana. Miaka ya karibuni mmoja wao akatembelea ofisi ninayofanyia kazi akiwa na cheo cha mkurugenzi, mteule wa rais. Mimi nilimkumbuka, na nilitaraji naye angenikumbuka lakini hata katika kutambulishana hakuonesha kukumbuka chochote. Baada ya kikao tuliwaandalia wakubwa lunch, huko nikasogea karibu naye zaidi lakini bado. Nikaona isiwe taabu bwana, asifikiri nataka kumzoea vibaya na cheo chake!
Natumaini Mzee Attas alipata wasaa wa kumsamehe mzee mwenzie huyo.
 
Huenda angemkumbusha angekula shavu..who knows
 
Kupata na kujitia umesahau au kuwasahau wana ni hulka tu ya mtu na ulimbukeni/tabia za kimasikini au Uzwazwa.

Binafsi mpaka leo hii nawakumbuka baadhi ya wana ambao nilikuwa nao sambamba tangu shule ya awali, sembuse Mwalimu eti alimsahau Mzee mwenzie aliyekuwa nae sambamba akiwa na umri wa miaka "30" (thelathini)

Duhh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…