Sharobaro maana yake nini?

Sharobaro maana yake nini?

Anko Sam

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2010
Posts
3,254
Reaction score
903
Wana JF, kuna kiswahili kimeingia kipya sifahamu maana yake kwa hakika. Kwenye majarida mbalimbali kila mwandishi analitumia kivyake nimeshindwa kupata maana halisi ya neno: Sharobaro!
 
Ewaalaaaah ambaye muda mwingi anautumia kwenye kioo,kwa kushindana na kinadada kwa urembo.
Kweli kabisa, wakat wanaume wa ukweli muda mwingi wanautumia kutafuta pesa. Hahahaha!.
 
Brazamen.....bishololo........shola.......bishoo.......etc!
 
Hii kitu ilishawahi kuelezwa hapa hapa JF

Sharobaro: Binti, Msichana, Mwamamwari, Kigori.

Na kinyume chake ni:

Barobaro: Mvulana, Kijana wa kiume, shababi.
 
Hii kitu ilishawahi kuelezwa hapa hapa JF

Sharobaro: Binti, Msichana, Mwamamwari, Kigori.

Na kinyume chake ni:

Barobaro: Mvulana, Kijana wa kiume, shababi.

Hivyo wanaojiita masharobaro maana yake tabia zao ni kama za mabinti? au labda mashoga?
 
Hivyo wanaojiita masharobaro maana yake tabia zao ni kama za mabinti? au labda mashoga?
Labda wamependezwa na ilo jina.

Ni sawasawa leo hii, ukimwita Mtu mke (Mwanamke) kwa jina la Dame, ataona kama umemzarau, wakati ili neno ni cheo (title), sawa na 'Sir'.
 
Wanaume shombe shombe wenyekupenda kujilemba sn kama mabinti tunaweza tukawaita mashoga japokuwa wanaekeiti.
 
Sharobaro ni utanashati. Hivyo mtanashati anaweza kuwa binti na hata mvulana pia.
 
ni mwanamme anaetaman kuwa mwanamke (kigori) na huwa mwisho wao huishia kuwa mashoga!!!


" ANYONE WHO VOLUNTEER FOR POLITICS SHOULD CONSIDER OTHERS FIRST
"
 
Back
Top Bottom