She wants to pay me "in kind"

She wants to pay me "in kind"

Salute Comrades!

Kuna hii ishu ambayo imenifikirisha sana mpaka nimeona niilete kwenu wadau mnipe mawazo yenu.

Yupo mwanamke mmoja ambaye anafanya kazi ya kuuza bidhaa mbalimbali kama vile mahindi, maharage, ndizi, karanga na mazaga zaga mengine Kama haya.

Basi huyu mwanamke Kuna kipindi alinifata dukani kwangu akaniomba nimkopeshe KSh 12,000 akaizungushe kwenye biashara Yake na akaahidi kuirudisha baada ya wiki 3.
Nikaona isiwe taabu ngoja nimsaidie huyu dada wa watu nikachukua 12000 nikamkabidhi bila hiyana akaenda.

Siku zikaenda wiki tatu alizoniahidi kunirudishia hell yangu nazo zikapita dada wa watu bado hastuki tu.Ikabidi nimkumbushie kuhusu Deni langu akaanza kuzuga zuga tu na kunipiga kalenda eti nisubiri kidogo ananiandalia hela yangu.

Mpaka nakuja kuomba ushauri wenu miezi miwili imepita Sasa lakini huyo dada bado ananizungusha hela yangu Hadi nimechoka kumdai.

Huyu mwanamke nimejuana naye tu kibishiara Kuna muda huwa naenda kwake kununua bidhaa mbali mbali kwa hiyo tumezoeana kibishiara tu Wala Sina uhusiano mwingine naye zaidi ya huu wa kibishiara na ukizingatia Ni ameolewa Ana mume na wamebarikiwa watoto wawili.

Sasa leo nimemfata Hadi kazini kwake nikamkoromea Sana na kumwambia anipe hela yangu nisepe sitaki mambo mengi amenikwamisha pakubwa Sana.Aisee mwanamke baada ya kuona hasira zangu amejishusha Sana na kunililia nimuonee huruma mixer kuniambia vijisababu mbali mbali eti ooh kwao walikuwa na msiba kwa hiyo muda huu Hana hela nimvumilie tu.

Nimeondoka nikiwa na hasira Sana kwa sababu sikutaks kuendelea kusikiliza ngojera zake.
Mwanamke aibu imemtoka akanitumia message ndefu Sana akaniambia ako tayari kunilipa penzi ili niweze kumsamehe Deni la pesa yangu.

Akaniambia Kama vipi nitafute lodge nzuri nilipie chumba anipe penzi ambalo mwenyewe anadai hajawahi kumpa mumewe hata siku moja.Baada ya kusoma huo ujumbe wake aisee nimechoka Sana na Ni dhahiri kwamba huyu mwanamke anataka kunikatili hela yangu mazima.

Wakuu, nitumie mbinu gani kumdai huyu mwanamke maana mi sitaki kuendekeza ujinga allioniambia kwa message na pia naheshimu Sana ndoa za watu.Nawaza niende kazini kwake nibebe bidhaa zitakazotosha kufidia Deni langu ila moyo unagoma nahisi nitakuwa namuumiza zaidi.

Pia nikifikiria kusaheme Deni la Ksh12000 naona haiwezekani kbsa hiyo Ni hela nyingi Sana.

Ushauri wenu utanifaa zaidi. Karibuni.
Imategemea kipato chako lakini elfu 12 sio hela nyingi ya kuja kuomba ushauri hapa. Busara ni kumsamehe kwani biashara haiku.muendea vizuri. Au kama ni rijali kubali akulipe penzi mbona utakuwa umepata mbususu kwa bei chee kabisa.

Usimfanyie ukatili wa kukamata bidhaa zake laana itakuandama.
 
Mbinu ni tatu tu na atakulipa pesa yako fasta

Hiyo sms ambayo ame kutumia kuwa yupo tayari kukupa penzi ambalo hata mme wake hajawahi kumpatia nenda nayo mpaka Kwa mme wake Na umuonyeshe, hiyo mbinu ya kwanza

Ya pili- mwambie kuwa kama hajakupa pesa yako kwenye wiki hii mtishie kuwa utaenda kumuonyesha mme wake hiyo sms

Ya tatu- lipia lodge kama alivyokwambia na mrekodi yaani mchukue video mkiwa mpo faragha kisha baada ya tendo muonyeshe hizo video mwambie asipokulipa pesa yako kuwa utatafuta namba ya mume wake na utamtumia hizo video

Chagua njia moja hapo Na ujipatie pesa yako fasta
Akifuata hiki unachomshauri atakuwa hana akili kabisa.

Kumfanyia unyama binadamu mwenzio tena mtu aliyekwama ni uwendawazimu.

Unapoamua kukopesha ujue unatake risk, hela inaweza isilipwe. Kama amekwama akulipe toka wapi?
 
Imategemea kipato chako lakini elfu 12 sio hela nyingi ya kuja kuomba ushauri hapa. Busara ni kumsamehe kwani biashara haiku.muendea vizuri. Au kama ni rijali kubali akulipe penzi mbona utakuwa umepata mbususu kwa bei chee kabisa.

Usimfanyie ukatili wa kukamata bidhaa zake laana itakuandama.
12000 Kenyan Shillings sio hela ndogo Kama unavyodhani mkuu.
 
12000 Kenyan Shillings sio hela ndogo Kama unavyodhani mkuu.
Angalia kati ya utu na hela nini kinakipa kwako zaidi lakini kumbuka hata wewe kuna siku utajakwama pia! So tumia utu, mkuu fanya kama ni mama au Dada yako huyo anayapitia hayo, je ungejisikiaje kumkuta anauza utu wake kisa deni,
 
Back
Top Bottom