Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
7SHEBE MOHAMED AWADH MZALENDO ALIYEHIFADHI HISTORIA YA TANU NA HISTORIA YA JULIUS KAMBARAGE NYERERE KWA JICHO LA CAMERA YAKE
Katika ukuta wa nyumba ya mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed kulikuwa na picha kadhaa za sisi watoto wake.
Katika picha zile kulikuwa na picha moja mimi nikiipenda sana. Ilikuwa picha yangu nikiwa na umri a kiasi cha mwaka mmoja hivi kwa hiyo picha hiyo ilipigwa mwaka wa 1953. Nimeshakuwa mtu mzima na nina shughuli zangu siku moja nilikwenda kumjulia hali mama.
"Mohamed hebu panda hapo juu tungua hizo picha zako."
Nikapanda kwenye kiti nikazitungua.
Mama akazifuta vumbi kisha akanambia, ''Chukua hizi picha zako kaanazo mwenyewe.''
Kwa wakati ule sikutambua kuwa alikuwa ananipa urithi wangu na kuniambia kuwa yeye hana muda mrefu tena hapa duniani kwa hiyo alitaka anipe zile picha zangu.
Haukupita muda mrefu mama akafariki.
Katika picha hizi mojawapo ilikuwa picha hiyo niliyoitaja hapo juu picha ambayo mimi nikiipenda sana na yeye akijua kuwa naipenda.
''Picha hii mama kanipiga nani?''
''Picha hiyo alikupiga Shebe,'' mama alinijibu.
''Shebe akikupenda sana siku moja alikuja akanimbia, ''Hebu nipe rafiki yangu nikampige picha.''
Mama yangu Bi. Mwanaisha alikuwa anakaa Mtaa wa Kipata na Livingstone na mkabala wa nyumba yake hii aliyokuwa akiishi ilikuwa studio ya Shebe Mohamed Awadh.
Mtoto wa Mzee Shebe, Mbaraka Shebe tulikuwa tukifanyakazi pamoja bandarini na nikimfahamu pia na dada yake Masad lakini sikujua kwa wakati ule kuwa baba yao alikuwa rafiki yangu toka nazaliwa.
Nilipomuuliza Mbaraka kama yeye ni mtoto wa Mzee Shebe aliyekuwa na studio Mtaa wa Livingstone na Kipata akaniambia ndiyo na huyo ndiye baba yake.
Nimepata kumzungumza Mzee Shebe hapa jamvini mara kadhaa lakini kama kupita njia.
Mzee Shebe Mohamed Awadh hajatajwa popote katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika lakini picha nyingi ninazoziweka hapa zinatoka katika jicho la camera yake katika miaka ya 1950 na naamini Mzee Shebe ni mtu wa mwanzo kuweka kumbukumbu za Nyerere na harakati za kupigania uhuru katika picha.
Baada ya uhuru Mzee Shebe aliajiriwa na magazeti ya TANU, ''Uhuru,'' na ''The Nationalist '' kisha akahamishiwa Maelezo na mwisho SHIHATA alikomalizia utumishi wake na kustaafu.
Mtoto wa Mzee Shebe Mbaraka ametunfanyia hisani kubwa kwa kutufungulia kasha la picha alizoacha baba yake nasi tuziangalie na hizi anasema ni chache tu lakini zinatosha kuturudisha nyuma nusu karne kuona wapi tulipotoka.
Mbaraka ameahidi In Shaa Allah kutochotea picha katika kasha la baba yake kadri siku siku zinavyosogea mbele.
Picha kushoto ni Shebe Mohamed Awadh, John Rupia na Julius Nyerere.