Shebe mpiga picha wa kwanza wa TANU na baba wa taifa mwalimu Nyerere

Shebe mpiga picha wa kwanza wa TANU na baba wa taifa mwalimu Nyerere

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074

Mzee Shebe

Picha hiyo hapo juu ya Mzee Shebe nimeiona leo asubuhi tarehe 2 Februari, 2018 baada ya kuwekwa FB na Adarsh Nayar mpiga picha maarufu.

Nasikitika kusema kuwa sijui mengi kuhusu Mzee Shebe ila kuwa alinipiga picha yangu ya kwanza hiyo hapo chini mwaka wa 1953 nikiwa na umri wa mwaka mmoja.

Picha hii kwa miaka mingi ilikuwa ikining’inia katika ukuta wa chumba cha mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed toka mimi napata fahamu ya utambuzi.

Katika miaka yangu ya utoto picha hii haikunihangaisha hadi nilipofika umri mkubwa na mimi kuwa na wanangu ndipo nilipoanza kuingalia kwa undani zaidi picha ile.

Lakini sikupatapo kutaka kujua ni nani alipiga picha yangu.
Siku moja nilimtembelea mama yangu Bi. Mwanaisha na nikamuuliza nani alinipiga picha ile.

Mama yangu akanambia kuwa picha ile anilipiga Mzee Shebe Mtaa wa Livingstone na Kipata ambako yeye alikuwa akiishi na mkabala wa nyumba yake ndipo Mzee Shehe alipokuwa na studio yake.

Mama akaendelea kunihadithia akisema kuwa iko siku Mzee Shebe alikuja nyumbani kuniangalia.

Mama anasema Mzee Shebe akiniita mimi rafiki yake.

Akamwambia mama kuwa amekuja kunichukua akanipige picha pale kwenye studio yake.
Picha ndiyo hii ambayo sasa inafika umri wa miaka 66.

Pale ilipokuwa studio ya Mzee Shebe hatua chache ilikuwa Kirk Street (Sasa Mtaa wa Lindi).

Mtaa wa Kirk Street kulikuwa na nyumba moja ya ukoo wa Sykes akiishi mama yao Abdul, Ally na Abbas Sykes, Bi. Mluguru bint Mussa.

Hii nyumba ina historia kubwa katika uhuru wa Tanganyika.
Miaka ya mwanzo ya TANU Nyerere alikuwa hapungui nyumba hii akifuatana na Abdul Sykes.

Bi. Mluguru alikuwa na nyumba nyingine Kipata Street kona na New Street (Sasa Lumumba Avenue) ambapo serikali ilijenga Cooperative Building miaka ya mwanzo ya 1960.

Serikali ilipotaka kununua nyumba zile ili ijenge Cooperative Building ambayo imeanza Kipata hadi Somali Street Mwalimu Nyerere alimwandikia Bi. Mluguru barua kumwomba akubali kuuza nyumba yake hiyo kwa serikali.

Nyumba hizi zilikuwa zikitazama Uwanja wa Mnazi Mmoja na ukivuka Somali Street kulikuwa na kiwanja cha TANU ambacho baadae TANU ilijenga jengo la Elimu ya Watu Wazima na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilianzia hapo.

Kirk Street akiishi Ramadhani Mashado Plantan mmoja wa wanachama wa African Association toka miaka ya 1930 na nyuma ya Kirk Street ulikuwa Somali Street alikokuwa akiishi Zuberi Mtemvu na Omari Londo wote hawa wanachama shupavu wa TANU.

Nyuma ya studio ya Mzee Shebe ulikuwa Kipata Street mtaa ambao alikuwa akiishi Ally Sykes. Kwa ufupi ni kuwa hii Gerezani kama mitaa ile iliyokuwa sehemu ilivyokuwa ikifahamika, ilikuwa sehemu inawaka moto kwa siasa za kudai uhuru.

Baadhi ya mikutano ya TANU ya miaka ile ya 1954/55 ilikuwa ikifanyika kiwanja cha Kidongo Chekundu kilichokuwa kinatazamana na Kiungani Street.

Mzee Shebe alikuwa mpiga picha maarufu katika mitaa yote ile na bila shaka hili ndilo liliomfanya yeye atokee na kuwa mpiga picha wa kwanza wa TANU na Baba wa Taifa Mwalimu

Julius Nyerere siasa za kudai uhuru wa Tanganyika zilipoanza 1954.
Kulikuwa na kijana mmoja sote tumeajiriwa na Bandari jina lake Shebe.

Siku moja nikamuuliza nani baba yake.

Katika mazungumzo akanambia kuwa baba yake alikuwa na studio Mtaa wa Livingstone katika miaka ya 1950. Hakika nilipata mshtuko.

Nikamwambia basi baba yake ingawa simkumbuki kwa sura kwa kuwa nilikuwa mtoto amenipiga picha ambayo ninayo mpaka sasa.

Nikamuuliza tena kama anamjua Masad Shebe.
Akanambia huyo ni dada yake.

Hii ilikuwa miaka ya 1980 na Masaad alikuwa akikaa Mtaa wa Livingstone na Mkunguni na akifanyakazi Air Tanzania.

Hivi sasa Masad ni Meneja wa Air Tanzania Zanzibar.

Nikazungumza Mengi na Shebe na yeye kwa kujua mapenzi yangu katika historia akanifanyia photocopy za picha nyingi sana alizopiga baba yake katika miaka ya 1950.

Bahati mbaya siku zile ‘’digital,’’ ilikuwa bado.
Hazina hii aliyoacha Mzee Shebe nimeihifadhi kama ilivyo katika Maktaba yangu.


Mwandishi, 1953
Picha aliyopigwa na Mzee Shebe
 
Mzee hongera kwa uandishi uliotukuka...lakini pia hongera kwa wazazi wako waliokulea vyema hata ukawa na afya A toka utotoni. Ila walisahau kukuvalisha shati ha ha ha
 
Mzee Mohamed,ilikuwaje Mwalimu toka bara akawa na influence kuliko watu karibu wote wa pwani!?..ina maana pwani hakukuwa na mtu mwenye upeo mkubwa mpaka wakaona yeye ndio awaongoze?
 
Mzee Mohamed,ilikuwaje Mwalimu toka bara akawa na influence kuliko watu karibu wote wa pwani!?..ina maana pwani hakukuwa na mtu mwenye upeo mkubwa mpaka wakaona yeye ndio awaongoze?
Wote wa pwani elimu dunia ilikua imewakalia kushoto....
 
Mzee Mohamed,ilikuwaje Mwalimu toka bara akawa na influence kuliko watu karibu wote wa pwani!?..ina maana pwani hakukuwa na mtu mwenye upeo mkubwa mpaka wakaona yeye ndio awaongoze?
Wise,
Fikra ya viongozi wa TAA toka chama kilipoasisiwa 1929 ilikuwa chama kiwe cha Watanganyika wote na Kleist Sykes kaeleza hili katika kumbukumbu zake alizoandika kabla ya kufariki 1949.

Tatizo ni kuwa Kanisa likiwakataza Wakristo kujiunga na harakati zozote za siasa.

Unaweza kuyasoma haya katika "Kleist Sykes:The Townsman," katika "Modern Tanzanians, (1973) John Iliffe Ed; historia iloyoandika na mjukuu wa Kleist, Daisy Abdul Sykes.

Sasa hiyo "influence," unayosema ya Nyerere hakuwa nayo katika siasa hadi pale alipochaguliwa kuwa rais wa TAA 1953 na TANU ikaundwa 1954.

Ukijua vipi TANU iliundwa na vipi Nyerere alikuja kupewa uongozi hizo fikra kuwa hapakuwa na watu wenye uwezo zitakuwa zimepata jibu.

Lakini kwa mukhtasari ninachoweza kukueleza ni kuwa nyuma ya Nyerere kulikuwa na viongozi "nationalists," kama Sheikh Hassan bin Amir, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes kuwataja wachache walioona mbali zaidi na kupanga mikakati ya umoja wa kitaifa kama silaha ya kuushinda ukoloni.

Ndiyo maana kama ulivyogusia kuwa iweje watu wa pwani wamuunge mkono Nyerere kutoka bara badala ya kumkata.

Wazee wetu walikuwa wanajua hatari ya ubaguzi na wakijua nguvu ya umoja.

Nimeandika kitabu kizima kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
 
Politburo,
Kwa nini unasema hii ni historia nyingine?

@ Mohamed Said namaanisha nimefurahia kusoma andishi/simulizi lako hili kuhusiana na huyu bwana mpiga picha. Masimulizi yako huwa yananivutia ndio kisa cha kusema hivyo
 
@ Mohamed Said namaanisha nimefurahia kusoma andishi/simulizi lako hili kuhusiana na huyu bwana mpiga picha. Masimulizi yako huwa yananivutia ndio kisa cha kusema hivyo
Politburo,
Ahsante kaka.
Jina lako inaelekea unawapenda Warusi.
Tafuta kitabu hiki: Khrushchev Remembers.

Hukiweki chini.
 
Mzee Mohamed Said hakika bila kumung'unya maneno unaifahamu sana historian ya nchi yetu.Unaonaje sasa uwe unaandika vitabu vingi zaidi ili iwe kumbukumbu ya vizazi vijavyo?
 
Politburo,
Ahsante kaka.
Jina lako inaelekea unawapenda Warusi.
Tafuta kitabu hiki: Khrushchev Remembers.

Hukiweki chini.

Shukrani, hakika nitakitafuta kitabu hiki. Napenda kuisoma historia yao tokea mapinduzi ua 1917 hadi usovieti iliposambaratika.
 
Back
Top Bottom