Ilankunda1234
JF-Expert Member
- Dec 28, 2015
- 4,841
- 4,797
Mkuu kwa miaka hiyo huyo mtoto hajawa na hadhi ya kuvaa nguo mkuu.Mzee hongera kwa uandishi uliotukuka...lakini pia hongera kwa wazazi wako waliokulea vyema hata ukawa na afya A toka utotoni. Ila walisahau kukuvalisha shati ha ha ha
Mwifwa,Shukrani sana kwa historia hii adhimu Mzee Mohamed Said.
Ya kale ni dhahabu.
Jungu kuu halikosi ukoko.
Sankara,
Maalim mohammad said
naomba kunijuza juu ya hiyo picha manake nakuona hapo kulia mtu wa nne kwa waliosimama ukiwa na rais Alhaj Ali Hassan Mwinyi
Kumbe we ni Mdogo wangu wa Mbali sana,Nasikitika kusema kuwa sijui mengi kuhusu Mzee Shebe ila kuwa alinipiga picha yangu ya kwanza hiyo hapo chini mwaka wa 1953 nikiwa na umri wa mwaka mmoja.
Slim 5,Hongera kwa kuweza kubaki na kumbu kumbu murua kama hii!
Hakika sheikh una historia adhimu sana. Allah akujaalie umri mrefu na tuwe na Mwisho mwema!Slim 5,
Hiyo picha ina historia nyingi sana inanikumbusha pia nilivyokuwa
mdogo mama yangu akiniwekea miziki ya Septet Habanero ya Cuba
tuko uani na gramaphone imewekwa kwenye kiti cha marimba.
Hii miziki ikipendwa sana na katika Sauti ya Dar es Salaam matangazo
ya radio yalipoanza mwaka wa 1952.
Nyimbo niliyokuwa nikiipenda sana inaitwa El Senor?
Sina hakika na hiyo spelling lakini ninayo CD Maktaba.
Basi mama ataniambia, Mohamed hebu waonyeshe hawa kucheza dansi.
Basi nitanyanyuka na kuanza kucheza.
Watu watacheka sana nilivyokuwa nalisakata Pachanga la Cuba.
Slim5,Hakika sheikh una historia adhimu sana. Allah akujaalie umri mrefu na tuwe na Mwisho mwema!
Zinc,mzee mohamed unanichekeshaga, ina maana akina mohamed huwaga mnapendaga utukufu kiac hiki au hii ni tabia ya mohamed ww km ww! mzee unapenda kutukuzwa kuliko hata Mungu wa Mbinguni, kila mada unayoleta ni aina ya watu flan flan wa kwako ww na unawaweka namba 1 kwamba hawa ndio walikuwa wa kwanza kwenye hiki na hawa walikuwa wa kwanza kwenye kile, ninaamini kabisa hata wale waliokuwa wanakuunga mkono mwanzoni washakuchoka, imebaki umri wako kwa sababu pengine wanakufahamu.
Zinc,mzee mohamed unanichekeshaga, ina maana akina mohamed huwaga mnapendaga utukufu kiac hiki au hii ni tabia ya mohamed ww km ww! mzee unapenda kutukuzwa kuliko hata Mungu wa Mbinguni, kila mada unayoleta ni aina ya watu flan flan wa kwako ww na unawaweka namba 1 kwamba hawa ndio walikuwa wa kwanza kwenye hiki na hawa walikuwa wa kwanza kwenye kile, ninaamini kabisa hata wale waliokuwa wanakuunga mkono mwanzoni washakuchoka, imebaki umri wako kwa sababu pengine wanakufahamu.
Mohamed Said: GEREZANI NA HARAKATI ZA UHURU WA TANGANYIKA SIASA KATIKA MJI WA DAR ES SALAAM MIAKA YA 1950Zinc,
Mimi namshukuru Allah kwa kote aliponipitisha.
Ninayohadithia na sehemu ya maisha yangu na wewe si wa kwanza kushangaa.
Najua kwa nini unataabishwa na historia hii.
Sababu ni kuwa katika akili yako umejenga fikra yako na hiyo haiendani na haya
unayosoma hapa.
Ukiwa unachoka kunisoma hakuna shida.
Ukiona post yangu unaipita unasoma ambayo hayakujakuchosa lakini ukweli ni
kuwa ni tabu sana kupuuza.
Wanaonitia moyo kuandika ni wasomaji wangu ambao wakiona post yangu wengi
watakuja na kuchangia.
Nimezaliwa Dar es Salaam ya 1950 Mtaa wa Kipata, Gerezani.
Sehemu ile katika Tanganyika ina historia kubwa sana.
Naingia Maktaba nitakuwekea link uisome historia hiyo.