Sheha Mpemba Faki, Mbunge mteule wa Konde (CCM) ajiuzulu

Sheha Mpemba Faki, Mbunge mteule wa Konde (CCM) ajiuzulu

Act wakishiriki Tena huo uchaguzi ntaamini maneno yako. Maana walituambia hawatashiriki uchaguzi
.... Act hawatakiwi kushiriki kipumbavu. Ni lazima kwanza ufanyike uchunguzi huru kubaini kilichotokea (kwa mujibu wa madai ya Act); wahusika wawajibishwe, n.k. Isiwe suala la kukimbilia jimbo na huenda CCM "wakajitoa" ili Act wapite bila kupingwa! Hii iwe case study.
 
Alama ya nyakati. Presha tactics iliyotumika ni ya hali ya juu. Hapa CCM wametambua hamna maslahi yao. Tusubiri wiki imalizike tuone yataisha vipi. Kwa kuwa jimbo ni la ACT, wamalize kuhesabu kura wampe mshindi kura zake. Haina haja kurudia uchaguzi wakati mshindi anajulikana.
 
ACT wametishia kujitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar, hivyo ccm wameona watazidi kuchafuka, hatimaye ikabidi wamtake huyo mbunge ajitoe kuepusha chama chao kuzidi kuchafuka.
ACT wananufaika na umoja wa kitaifa maana wamepata mawaziri mpaka makamu wa Rais
 
Bado hawajafanya kitu kwani uchaguzi utarudiwa na ACT walisema hawatashiriki tena chaguzi labda wakengeuke hivo bado CCM watatangazwa washind, kiufupi CCM ninaona kama inaelekea mwisho hivi
ACT wametishia kujitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar, hivyo ccm wameona watazidi kuchafuka, hatimaye ikabidi wamtake huyo mbunge ajitoe kuepusha chama chao kuzidi kuchafuka.
 
HONGERA Sana ustadhi,waislamu si watu wa dhulma.umekuwa mkweli rehema zake Mungu ziwe juu yako na wengine wafuate nyayo zako.
 
Haki huinua taifa Bali dhuluma huleta damu katika taifa
 
2 Aug 2021
Unguja, Zanzibar

Rais Mwinyi leo amuapisha Mkurugenzi mpya wa ZEC na makatibu wakuu



Source : Weyani Tv
.
Agosti 2, 2021

Huku CCM Zanzibar yashangazwa na kujiuzulu kwa mbunge wake mteule wa Konde, Pemba Zanzibar, ndugu Sheha Mpemba Faki


Bashir Nkoromo, CCM Blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeelezea kusikitishwa kwake na hatua ya aliyekuwa Mbunge wake mteule wa Jimbo la Konde Pemba, Visiwani Zanzibar Shekha Mpemba Fakhi kujiuzulu baada ya kuchaguguliwa katika Uchaguzi mdogo uliofanyika Julai 18 mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekua Mbunge wa jimbo hilo Khatibu Haji.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, imesema CCM imepokea barua ya Mbunge huyo kujiuzulu, Mbunge huyo akieleza kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia jambo ambalo Shaka amesema Chama hakina uwezo wa kumzuia hasa ikizingatiwa kuwa ni haki yake ya Msingi kama ilivyo kwa haki ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM. Ifuatayo ni taarifa ya CCM kuhusu Mbunge huyo kujiuzulu.
1627910431015.png

Picha toka maktaba: Mbunge wake mteule wa Jimbo la Konde Pemba, Visiwani Zanzibar Shekha Mpemba Fakhi
 
Bado hawajafanya kitu kwani uchaguzi utarudiwa na ACT walisema hawatashiriki tena chaguzi labda wakengeuke hivo bado CCM watatangazwa washind, kiufupi CCM ninaona kama inaelekea mwisho hivi

ACT walisema hawatashiriki wakati wameshiriki boss?
 
Nasubiri kwanza uchaguzi urudiwe akishinda mgombea wa ACT ndio nitajua cha kuandika, kwa sasa bado mapema.
 
Kama CCM wameamua kuachia then wasisimamishe mgombea kwenye uchaguzi mdogo kuokoa ghalama... Wizi wao tayari ushalitia Taifa hasara.
 
Kweli hapo tu ndipo nawapendea islams sio mipuuzi Mwigulu wanaua watu kisa siasa.....kesho front row kanisani..mwanafikiii
 
Pongezi kwake ni nadra sana tena sana kiongozi kujiuzulu Hapa Tanzanua au Afrika na kuachia ulaji hasa nyakati hizi za maposho, mishahara minono nk
 
Back
Top Bottom