Shehe Ponda aliamsha, adai Mashehe 300 wameswekwa rumande miaka 10 bila kesi

Shehe Ponda aliamsha, adai Mashehe 300 wameswekwa rumande miaka 10 bila kesi

Taarifa iliyotolewa na Shehe mwenye ushawishi mkubwa sana kwenye eneo la maziwa makuu, Ponda Issa Ponda na kunukuliwa na gazeti la Raia Mwema, anaeleza kwamba kuna zaidi ya mashehe 300 waliorundikwa rumande bila kupelekwa mahakamani kwa zaidi ya miaka 10.

Bali haijafahamika sababu hasa ya kuwakamata viongozi hao wa kiroho na kuwaweka kizuizini kwa miaka yote hiyo bila kuwasomea mashtaka yanayowakabili na wala haijulikani kama wote hao wanatuhuma zinazofanana ama la.

View attachment 2346464

Chanzo: Raia Mwema
Shekh Mtumishi wa Mungu na wanadamu. Shekhe mwenye baraka zake kwa Mungu.
 
We have to be careful hapa, tusichukue advantage tu ya kuwa Rais huyu ni Mwisilamu basi atatoa kauli. Ninavyojuwa kazi ya She iko Msikitini kuongoza ibada mbalimbali. Mpaka uone Serikali hasa wakati wa JK Mwisilamu mwenzao akiwaweka ndani ujue taarifa zao zilikuwa za hatari.

Toka Hawa watu wawekwe ndani uchomaji makanisa na kuua mapadri kulikoma. Kama tungecheka na nyani basi hawa Alshabab wangetusumbua kama walivyoisumbia Mozambique
Hizo zilikuwa porojo za ccm iliyofeli tangu enzi zile. Naona na wewe uliingizwa mkenge kwa propaganda.
Ccm ilizidiwa na CUF wakaanzisha vita hiyo ya kiimami ili kuwadhofisha. Bara huku walishindwa walikutana na visiki vya mpingo hadaa zikafeli
 
CUF inaingiaje hapo? Yaani Shehe unaacha kazi zako za kuongoza roho za wanadamu unaanza mambo ya siasa?
 
CUF inaingiaje hapo? Yaani Shehe unaacha kazi zako za kuongoza roho za wanadamu unaanza mambo ya siasa?
Kwani walipoimba chadema na wakristo ulikuwa wapi?
Ccm with its all instruments can do anything, say anthing ili iendelee kutawala bila kujali damage itakayotokea kwenye jamii.
 
Back
Top Bottom