Shehe Shariff Majini kulalamika kaibiwa kura Tanga, je majini yake hayamlindi?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau.

Mtia nia maarufu kama shehe sharif majini analalamika uchaguzi wa kura za maoni jimboni kwake haukuwa wa haki.. na ameshindwa kwa mbinu chafu.

Swali nalojiuliza. je majini hayana msaada ya kumlinda mtu wao asiibiwe kura?

Je, kina sisi tunaopeleka shida zetu kutatuliwa kwa nguvu za majini yake huwa tunatapeliwa?
 
Mbuzi kalamba chuma cha reli..hawa manabii na masharifu wangetulia kwenye mishe zao tu kuliko kuingia kwenye anga za siasa maana siasa ni mchakato mkali.ona sasa wamejiharibia madili yao kwa watu wao wanajipiaga mpunga.kumbe kwenye siasa hakuna njia mkato hata ya kinabii wala kisharifu ni full kupiga domo na kuongopa kwa saana....
 
Tapeli katapeliwa.
 
Huyu jamaa kesha jibandika mwenyewe bango kwamba yeye ni tapeli, sijawahi kuwaamini kabisa watu dizaini hii pamoja na wale wanaojiita manabii na mitume.
 
Kwani jamani mbona hata wenye pesa unakuta analilia mapenzi au hali vyakula vitamu kisa maradhi wakati tunaambiwa pesa ndio kila kitu,na hawa nao tusiwapime kuwa wanaweza kila kitu.
 
Reactions: Tui
Mganga kazi yake kuagua/kutibu matatizo mbali mbali haswa matatizo ya nguvu za giza .

Pia kumbuka mganga hajigangi.

Ukielewa haya mawili hutopata shida kuwaelewa waganga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…