Shehena ya Bangi yanaswa Arusha ikisafirishwa nchi jirani

Shehena ya Bangi yanaswa Arusha ikisafirishwa nchi jirani

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Shehena ya Bangi yanaswa Arusha ikisafirishwa nchi jirani

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekamata shehena ya Bangi inayokadiriwa kufikia magunia 15 yakisafirishwa kwenda nchi jirani kwa kutumia gari dogo la abiria aina ya Noah.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Salumu Hamduni amesema bangi hiyo imekamatwa katika Kijiji cha Albomba wilaya ya Longido baada ya polisi kulitia shaka gari hilo na kuanza kulifuatilia.

Kwa mujibu wa Kamanda Hamduni wakati polisi wanafukuza gari hilo linalofanya safari zake kati ya Arusha na Namanga lenye namba za usajili T302BXZ ilipata pancha na dereva akalitelekeza akakimbia japo alikamatwa baada ya saa sita kufuatia msako mkali ulioendeshwa na Jeshi la Polisi.

Aidha kamanda Hamduni amewapongeza na kuwashukuru askari waliofanikisha kukamata bangi hiyo na kwamba taratibu za kuwapa zawadi kama motisha wa kuonyesha uadilifu na utendaji kazi mzuri na uliotukuka.

"Askari wote wanafanyakazi nzuri lakini wapo wanaojituma zaidi ,hawa utaratibu wa kuwapa motisha uko wazi na utafuata ,na kumbuka kuwa zawadi za motisha ziko nyingi sio lazima fedha"alisema Kamanda Hamduni.

Kamanda Hamduni pia amewapongeza viongozi wa wilaya ya Longido kwa ushirikiano mkubwa wanaotoa kwa jeshi la polisi katika kukabiliana na uhalifu .

"Haya ni moja ya matunda ya ushirikiano wa watendaji wa Halmashauri ya wilaya hii na vyombo vya dola,na huu ni mfano unaotakiwa kuigwa na wilaya zingine"alisema Kamanda Hamduni.

Awali mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe amesema pia mafanikio hayo yamechangiwa na ushirikiano unaotolewa na wananchi wakiwemo walinaoishi maeneo ya mpakani.

"Kwa muda mrefu sasa tumekuwa na kazi kubwa ya kuwaelimisha wananchi wa vijiji vya mpakani na nchi jirani juu ya umuhimu wa kutoa ushirikiano ukiwemo wa taarifa za wahalifu na kwa sasa asilimia kubwa wanatoa taarifa"alisema Mwaisumbe Dc Longido .

Shehena hiyo ya Bangi imekamatwa ikiwa ni siku chache baada ya bangi nyingine kukamatwa katika wilaya ya Arumeru tukio ambalo lilipelekea baadhi ya watendaji kuwajibishwa.

Kwa mujibu sheria gari ama chombo cha moto kitakachokamatwa na dawa za kulevya kinataifa jambo linaloonyesha kuwa basi hilo dogo kwa sasa kitataifishwa .

Licha ya kuwepo kwa matukio kadhaa ya matumizi ya magari ya abiria kusafirisha madawa ya kulevya ,tukio hili la kutumia basi dogo aina ya Noah ni la Kwanza katika wilaya ya Longido na pia mkoa wa Arusha.

Chanzo: ITV
 
Polisi wetu mkikamata bangi inakwenda nje ya nchi iachieni tu kama hamjaiona cha muhimu tu iwe biashara ya Mtazania na imetoka ndani ya Tanzania, Mkikamata bangi na madawa mengine yanaingia Tanzania yakamateni na mhusika peleka jela, mkigundua huo mzigo uko transit chukueni chenu na muupe escort mpaka unavuka border...

Mkiona bangi inalimwa mahala ndani ya Tanzania, hakikisheni mkulima hauzi ndani ya Tanzania bali anapeleka nje ya Tanzania...
 
Ni vyema bangi ikaruhusiwa kulimwa Tanzania lakini iwe kwa export business na matumizi ya ndani yapigwe marufuku, anayeitaka aje aichukue huku akauze nje ya Tanzania na iwe marufuku mashamba kumilikiwa na wageni na kama wanalima basi hisa iwe 50/50 na Mtazania na operations zifanywe na Watanzania.... this is the opportunity purposely for our people economy.
 
Ni ngumu sana ku control ulimaji na uuzaji wa huu mmea. Labda taasisi za serikali ndio zifanye hicho kilimo, ila ikiwa ni kampuni tu hivi na kuajiri watu lazima mjani usambae mtaani.

Wapewe JKT na Magereza, walime mmea na ku process bidhaa zote za mjani ready for export.
 
Polisi wetu mkikamata bangi inakwenda nje ya nchi iachieni tu kama hamjaiona cha muhimu tu iwe biashara ya Mtazania na imetoka ndani ya Tanzania, Mkikamata bangi na madawa mengine yanaingia Tanzania yakamateni na mhusika peleka jela, mkigundua huo mzigo uko transit chukueni chenu na muupe escort mpaka unavuka border...

Mkiona bangi inalimwa mahala ndani ya Tanzania, hakikisheni mkulima hauzi ndani ya Tanzania bali anapeleka nje ya Tanzania...
Na Mkulima Apewe Leseni Kama Wanavyopewa Wamiliki wa Silaha, ili akivurunda huu utaratibu unaouelezea iwe rahisi kumkamata. SORRY MKUU, NILIKUWA NAKAZIA POINT YAKO.
 
Huo mzigo wakitaka wauteketeze waite Machalii ya R kama 1000 kila mtu alikoki,ndani ya masaa sita watakuwa waneshamaliza.
 
Back
Top Bottom