Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir, amewataka Waislamu Nchini kufunga kwa siku tatu kuanzia kesho hadi Jumamosi, huku wakimuomba Mwenyezi Mungu aliepushe Taifa na mabalaa na kulijalia mvua yenye kheri na baraka.
Wito huo umetolewa kufuatia tahadhari za hali ya hewa, ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa kuhusu uwezekano wa hali ya El Niño, inayoweza kuathiri mwenendo wa mvua katika maeneo mbalimbali Nchini.
Sheikh Zubeir amewataka Waislamu kutumia siku hizo tatu kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa dua na ibada, wakimuomba aliepushe Taifa na majanga, maafa na mabalaa, huku mvua zitakazonyesha zikiwa za manufaa kwa Wananchi, mifugo, kilimo na mazingira.
View attachment 3666717
Kumuomba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, azuie janga hili ili watu wake wasipatwe na maafa, ni contradiction.Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir, amewataka Waislamu Nchini kufunga kwa siku tatu kuanzia kesho hadi Jumamosi, huku wakimuomba Mwenyezi Mungu aliepushe Taifa na mabalaa na kulijalia mvua yenye kheri na baraka.