TANZIA Sheikh Ahmed Haydar, Imam wa Masjid Mwinyi Kheri Akida afariki dunia

TANZIA Sheikh Ahmed Haydar, Imam wa Masjid Mwinyi Kheri Akida afariki dunia

Shaikh Ahmad Haidar Mwinyimvua
Katika miaka ya 50 kuendea 60 alikua mwanafunzi wa Muslim Academy Znz. Akasafiri kwenda Aden kabla ya kwenda Misri . Huko Misri alisoma miaka 13 .
Alikua mwalimu hodari wa Sharia na Lugha ya Kiarabu.
Aliwahi kwenda Mzumbe Morogoro kuwasomesha Mahakimu Ndoa na Mirathi ya Kiislamu. Baadae alikua ni Imamu wa Msikiti wa Mwinyi Kheri Akida. Hapo alidumu mpaka kufariki kwake.
Aliugua ugonjwa wa Kisukari. Alikua ni mkweli na mwenye uchungu wa Dini yake. Mara nyingi akituhimiza kusoma sana. Aliwahi kisomesha Lugha ya kiarabu Elimu ya watu wazima katika shule ya Gerezani. Mie nilikua ni mmoja katika wanafunzi wake aliowasomesha Lugha ya Kiarabu. Allah amrehemu na ajaalie kaburi lake linawirike kwa nuru ya elimu
Poleni sana.
Ile lugha iliyoandikwa kwenye Quran ni lugha gani?lugha ya asili ya Quran.
 
Back
Top Bottom