PreGE2025 Sheikh Akilimali: Tudumishe amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

PreGE2025 Sheikh Akilimali: Tudumishe amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
418
Reaction score
550
Sheikh Rashid Akilimali, Sheikh wa Mkoa wa Rukwa, amewahimiza wananchi kudumisha amani na utulivu wakati taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Ametoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuunganisha Watanzania bila kujali tofauti za kidini, kikabila au kijamii, akisisitiza kuwa uongozi wake umetanguliza maridhiano, mshikamano na maendeleo kwa wote.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Sheikh Akilimali amewataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa kupuuza siasa za kiharakati zisizo na tija kwa taifa, akisema siasa hizo mara nyingi hulenga kuchochea migawanyiko na kuvuruga amani iliyopo.

Amesema uchaguzi ni mchakato wa kidemokrasia unaopaswa kuendeshwa kwa amani, busara na kuheshimiana. Amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi kwa njia ya utulivu, huku wakilinda amani ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli.

 
Huyu Shekhe hakemei uporaji wa kura ndio utakaoleta machafuko akemee waporaji ambao ni hao CCM.
 
Ni kazi ngumu sana kuwatenganisha Masheikh wa Bakwata na CCM! Ahueni wale Masheikh wa Shura ya Maimam wakitoa tamko lao, unakuta mara nyingi lina mashiko. Ila siyo hawa Masheikh wa Bakwata.
 
Huyu Shekhe hakemei uporaji wa kura ndio utakaoleta machafuko akemee waporaji ambao ni hao CCM.


Huyo atakuwa miongoni mwa wale mashekhe tulioambiwa wanatembea na majini mfukoni.

Shekhe wa kweli ni Ponda, mpigania haki wa kweli, siyo haya machawa.
 
Huyo atakuwa miongoni mwa wale mashekhe tulioambiwa wanatembea na majini mfukoni.

Shekhe wa kweli ni Ponda, mpigania haki wa kweli, siyo haya machawa.
Sijamsikia SHEIKH PONDA ISSA PONDA kwenye hii Kampeni ya NO REFORMS NO ELECTION

Tunaomba Kampeni ikifika Kanda ya Pwani Boniyai asiache kumualika Sheikh Ponda Issa Ponda Majukwaani.
 
Back
Top Bottom