Sheikh Rashid Akilimali, Sheikh wa Mkoa wa Rukwa, amewahimiza wananchi kudumisha amani na utulivu wakati taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Ametoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuunganisha Watanzania bila kujali tofauti za kidini, kikabila au kijamii, akisisitiza kuwa uongozi wake umetanguliza maridhiano, mshikamano na maendeleo kwa wote.
Sheikh Akilimali amewataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa kupuuza siasa za kiharakati zisizo na tija kwa taifa, akisema siasa hizo mara nyingi hulenga kuchochea migawanyiko na kuvuruga amani iliyopo.
Amesema uchaguzi ni mchakato wa kidemokrasia unaopaswa kuendeshwa kwa amani, busara na kuheshimiana. Amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi kwa njia ya utulivu, huku wakilinda amani ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli.
Ni kazi ngumu sana kuwatenganisha Masheikh wa Bakwata na CCM! Ahueni wale Masheikh wa Shura ya Maimam wakitoa tamko lao, unakuta mara nyingi lina mashiko. Ila siyo hawa Masheikh wa Bakwata.