Sheikh Alhad Mussa Salum huna ubavu kuufunga mjadala huu

Sheikh Alhad Mussa Salum huna ubavu kuufunga mjadala huu

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,935

Nimemsikiliza huyu aliyewahi Kuwa sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, almaarufu Alhad Mussa Salum.

Amekuja na tamko la hiyo wanayojiita kamati ya maridhiano na amani. Anaongea kinafiki, akiomba viongozi wa Dini kutorushiana maneno kutokana na kadhia ya mkataba wa DP-WORLD.

Ameenda mbali na kusema sasa yete na kamati yake,wanaufunga mjadala na anaomba tuiachie serikali itimize wajibu wake kutokana na maoni ya wananchi kutosha sasa.

Sasa nikashindwa kumuelewa. Kwa sababu mpaka sasa hakuna viongozi wa Dini waliorushia maneno wenzao, zaidi ya masheikh kadhaa wanaoibuka na taasisi zao tofauti za kiislamu toka huko watokako.

TEC walikwishamaliza kazi yao na sasa waraka unatembea kwa kasi ya 5G.
Yeye Sheikh Alhad angeacha kuzunguka mbuyu na awaambie wenzake waache upotoshaji bali waujadili mkataba husika na waseme vifungu wanavyoviunga mkono ili jamii iwaelewe.Badala ya kuja na hoja za Udini bila mkataba mkononi kama walivyofanya wenzao wasomi wa TEC.

Nguvu inayotumika inaiaibisha serikali.
Sasa Serikali imefikia hatua mnatuletea hadi Masheikh walioondolewa madarakani kwa kashfa za kuingilia ndoa za kina Dk Mwaka?

Masheikh ambao walikuwa wakijibizana na kina Mange Kimambi?

Kweli Deep World?
Mungu inusuru Tanzania [emoji1241]
 
Huyo Sheikh Mussa alhad hana tena legitimacy ya kutuongelea watanzania sababu alikwishaingia kwenye kashfa nzito iliyopelekea kuondolewa katika wafhifa wake wa kuwa sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam.

Ingekuwa nchi za wenzetu, huyu hawezi hata kuruhusiwa kushika mick kuongea kwenye jamii.
 
So hao masheikh walisubiri tamko la TEC ndiyo waongee?

Mbona kulikua na makundi ya watu wengi tu wakipinga mkataba hata before hao TEC.
Why wasubiri tamko la TEC ndiyo na wao warespond?

In fact sijaona dini zikijibizana.
Ni mhemko tu wa kundi fulani.
 
Mzee wa upako nae yuko live Mwanahabari Digital
 
Deep World indeed.

Muhimu waseme vifungu wanavyoviunga mkono na wanavyovipinga. Hoja yao ni ipi hasa? Tusiangalie dini, udini, Nani ametoa Waraka, hoja zao ziko sawa?

Pia kama kunakosa lolote kwenye Waraka wa TEC watuambie.

Waraka una mantiki, umesimama na kusimamia maslahi ya Watanganyika na Watanzania.
 
Huyu jamaa si aliondolewa kama mwwnyekiti na badala yake mwenyekiti kawa sheikh wa mkoa wa dar ..?

Imekuwaje tena arudi kuwa na cheo ambacho hana ..?
Mkuu CCM kwa ajili ya DP-WORLD iko radhi hata kumtoa jambazi aliyefungwa Gerezani ili mradi tu wamtumie kupipitisha agaenda yao.

Sisi tunachukulia kawaida ila kwa wana CCM kundi wahuni,wako vitani hasa tena ukizingatia kwamba 6ayari wameishapokea kishika uchumba na pia kuna tetesi kwamba ile ndege yetu ya Rais imeshikilowa Dubai.
Kisa ni pesa y Deep World waliyokwisha itoa kuwa na thamani kubwa kuliko hata hiyo ndege yenyewe.
 
Unakosa uvumilivu Lisa hupend kusikia usiyoyapenda.
Kaufunga mjadala ndio shida IPO WAP.
 
Mkuu CCM kwa ajili ya DP-WORLD iko radhi hata kumtoa jambazi aliyefungwa Gerezani ili mradi tu wamtumie kupipitisha agaenda yao.
Sisi tunachukulia kawaida ila kwa wana CCM kundi wahuni,wako vitani hasa tena ukizingatia kwamba 6ayari wameishapokea kishika uchumba na pia kuna tetesi kwamba ile ndege yetu ya Rais imeshikilowa Dubai.
Kisa ni pesa y Deep World waliyokwisha itoa kuwa na thamani kubwa kuliko hata hiyo ndege yenyewe.
CCM wako radhi kuua ili DPW ipite
 
Huyu jamaa si aliondolewa kama mwwnyekiti na badala yake mwenyekiti kawa sheikh wa mkoa wa dar?

Imekuwaje tena arudi kuwa na cheo ambacho hana?
Hakuna mwenye afadhali hapo
FB_IMG_16929595310560830.jpg
 
Back
Top Bottom