kibobori mahoro
JF-Expert Member
- Dec 12, 2022
- 7,452
- 10,785
Kama kawaida yake uislamu ni dini ya haki na isiyotoa mwanya wa ujanja,utapeli na unyonyaji.
Masheikh mbali mbali wameendelea kuweka wazi msimamo huo wa uislamu ambao umo kwenye Qur'an na suna za mtume Muhammad rehma na amani zimshukie.
Katika ufafanuzi huo,masheikh wamesema kama itatokea muislamu kulazimishwa na mifumo ya kiinchi kuchangia bima kwa lazima basi siku atakapoumwa na ikatibiwa kwa gharama zaidi ya zile anazochangia kwa mwaka basi ni wajibu kwake kuuliza hesabu hizo na tofauti ya juu aliyokuwa hakuchangia basi aitoe sadaka.
Muhimu kuliko yote asitibiwe kwa pesa walizochangia wengine.Atibiwe kwa pesa zake mwenyewe au zilizochangwa na ndugu na wahisanai wake.
View: https://www.youtube.com/watch?v=OjIHAm_536s
Kama sijaelewa vile!nahitaji ufafanuzi.