Madrid,
Hili unaloeleza si jambo la kawaida.
Kawaida ni kama nilivyoeleza na kuweka hapa mifano halisi.
Nimgependa kujua alipokatwa baba yako hiyo nafasi yake alipewa nani?
Unajua Mo swala siyo kapewa nani mzee wangu.Unajua ukija na mantiki ya kusema waislam wameonewa unakosea Kwa sababu hata wakristo nao walipitia majanga Mimi mwalimu secondary aliniambia yeye alikua yuko vizuri darasan akafeli mtihani wa mwisho akarudia darasa mara mbili hakuchomoka kabisa.
Ikabidi akapambana akaenda shule ya wakatoliki wakaona mbona kijana yupo Vizuri tu.Anakwambia enzi zao unaweza ukarudia hata mara 4 na usipate nafasi.
Mzee wangu shule aliyosoma alifaulu mwanafunzi 1 tu wilaya nzima hawa Fiki 10.Mi naamin ukweli unajua sema unajaribu kuupindisha.[/QUOTE]
Madrid,
Nakuwa na subira kwa kuwa najua wewe huijui historia ya Waislam baada ya uhuru.
Mimi nina wajibu wa kukusomesha hadi ujue hata kama hukubaliani na mimi.
Umesoma kitabu cha
Abdul Sykes?
Kila aliyekisoma kitabu hicho alitoka kabadilika.
Hebu tuanze hapo kwanza.
Usije na kesi moja ikawa umejenga hoja.
Nadhani umesoma mikasa ya wanafunzi wa Kiislam na Wizara ya Elimu nilizoweka
hapa.
Nakuongezea mkasa mwingine:
Mwalimu Bori Lilla alikuwa mwalimu Mkuu wa shule mbalimbali kwa miaka mingi.
Mzee Lilla alikuwa katika Kamati ya Kusahihisha Mitihani.
Baada ya kumaliza kusahihisha wakawa sasa wanaweka majina halisi badala ya no.
ili wanafunzi wafahamike.
Katika orodha yao kulikuwa na idadi kubwa tu ya wanafunzi Wakrsito na Waislam.
Mmoja wanakamati akaona orodha ya
Mzee Lilla ina Waislam wengi akauliza kwa
sauti kali: ''Mbona orodha yako imejaa Waislamu?
''Wewe mgeni humu ndani?
Mzee Lilla akamjibu kwa sauti kali vilevile, ''Mimi siyo mgeni mimi Muislam.''
Ukimya ulitokea pale ulikuwa mkubwa.
Mzee Lilla haya kanihadithia kwa ulimi wake mwenyewe.
Ninaandika haya ili nyie msiojua kuwa lipo tatizo mfahamu na viongozi wetu
nao pia wajue ili watumie madaraka yao kuondoa dhulma katika nchi yetu
kwani dhulma ikiachiwa ishamiri huangamiza.