Sheikh Hamisi Mataka: Nilivyokoseshwa elimu ya Sekondari

Sheikh wangu,
Sina uhakika kama nimefanikiwa kukuonesha tunachotofautiana katika huu mjadala. Ngoja nijitahidi kueleza kwa kifupi.
Nakubaliana na wewe kiasi kikubwa kwa mambo makuu mawili:
  1. Historical facts unazotoa. Nyingi hazina ubishi, na hakika tunaelimika kusoma kuhusu hayo matukio mbalimbali uliyoeleza katika kitabu chako (nimekisoma chote) yaliyotokea wakati wa harakati za uhuru, na za wahusika wake. Kama mtu alishiriki harakati fulani, hiyo ni fact, haiwezi kubadilishwa ikasemwa hakushiriki. Kama mtu alitoa mchango fulani, haiwezekani kukanusha na kudai hakutoa, hata kama ikikanushwa ukweli haubadiliki ukawa uwongo kwa kuwa kuna watu wamekanusha.
  2. Vyanzo unavyotumia na kuhakiki taarifa zako vipo, na ni traceable, hata mwingine akifuatilia atahakiki.
Ninatofautiana nawe mambo kadhaa lakini hapa nataja moja kuu: ingawa unaeleza matukio ya kweli, unayapa maelezo ama sababu zisizothibitishwa ukweli wake, na hiki ndicho chanzo cha farka.

Nikupe mfano kwa kunukuu sehemu ya sentensi yako ya kwanza hapo juu. Umesema "..........EAMWS ilivunjwa kwa kuwa ilikuwa na mipango imara ya kuwanyanyua Waislam......." Sentensi hii ina tunachokubaliana na tunachotofautiana.

EAMWS ilivunjwa (hii ni fact, tunakubaliana) kwa kuwa ilikuwa na mipango imara ya kuwanyanyua waislam (hapa tunatofautiana. Ushahidi wa hili uko wapi?) Hao waliovunja hiyo taasisi walitoa sababu gani, na je hizo sababu zina ukweli au uongo gani? (kwa ushahidi). Je taasisi nyingine zilizokuwa zinawanyanyua waislamu nazo zilivunjwa, au hazikuwepo? Waislamu walikatazwa au kuzuiwa kuunda taasisi nyingine yenye malengo yaleyale ya kuwanyanyua waislamu?

Hiyo conclusion ya kuhusu sababu ya kuvunjwa kwa taasisi hiyo huna data za kuithibitisha.

Kwa hakika nakusifu kwa uandishi mzuri wa kiswahili na kiingereza, na nimekusikia ukizungumza lugha zote mbili kwa umahiri kabisa. Simulizi zako kuhusu yaliyotokea na yalivyotokea hazipingwi kwa kuwa kwa kiasi kikubwa ni za kweli. Kwenye zile za "What happened, when, where, by who and how" uko vizuri. Tatizo liko kwenye "why", hapo ndipo unapotuingiza chaka mzee wangu.
 
Ralph...
Mimi kutoa ushahidi wa aina ya mahakama sitaweza nitabaki kwenye utafiti tu
ambao wewe huukubali.

Ila nimeshukuru kuwa umetimia neno, ''shaka.''
Shaka inaweza ikawa kweli au vinginevyo.

Hapa ndipo penye uzuri wa shaka.

Yapo mengine siwezi kuandika hapa lakini ikiwa In Shaa Allah itatokea siku mimi
na wewe tukakutana uso kwa macho nitakueleza na wala si nia yangu ukubali kuwa
nasema kweli, la hasha nia ni kutaka ujue kuwa hili nalo limesemwa hata kama wewe
hutaamini.

Upo ushahidi wa Rashid Kayugwa nimemweleza kwa undani katika kitabu na pia
uko ushahidi wa Geoffrey Sawaya na yeye nimemweleza katika kitabu cha Abdul
Sykes.


Lakini upo ushahidi wa Sivalon ambao ni maarufu.

Upo pia ushahidi wa Bergen ambao baada ya kuonekana aliyoandika ni maneno mazito
Cathedral Bookshop ambao ndiyo walikuwa wasambazaji wa kitabu hicho hawakiagizi
tena.

Naamini kuwa unazo taarifa pia kuwa mchapaji wa wa Sivalon Ndanda na wao pia kitabu
hiki wamekizuia na hizo nakala unazoona zinauzwa nje ya misikiti ni vijana wajasiriamali
wanachapa kwa njia zao wenyewe kujitafutia riziki.

Ushahidi wa Njozi haukuweza kuwafikia wananchi kwa kuwa kitabu kilipigwa marufuku.
Ukikutwa na kitabu hicho ni kosa la jinai.

Ralph,
Nakushukuru sana kwa uungwana wako na kwa hakika unakisukuma kichwa changu
kufikiri tofauti na wenzangumie humu ambao huishia kunitukana.

Napenda kumaliza kwa kukueleza kitu.

Marehemu Prof. Haroub Othman aliumizwa sana na kitabu changu na cha Ali Muhsin
Barwani
kiasi alimkabili Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akamuomba atoe
majibu ya yale tuliyoandika kuhusu historia ya nchi yetu ili ukweli ujulikane.

Prof. Haroub alitaka Baba wa Taifa athibitishe au akane yale yaliyoandikwa.
Kwake huo ndiyo ungekuwa ukweli lakini hakuweza kutuamini sisi wawili.

Huwa sishangai watu wanaponikanusha.
 
Huo ndio uhalisia, lengo ni kukatisha tamaa lakini kwakua hakuweza kukata tamaa, alipambana mpaka damu ya mwisho kuona aalichokitarget kinafanikiwa....
Kwahiyo huko mbele alikoendelea alisomea madrasa au kwa wale wale unaosema walikuwa na lengo la kumkatisha tamaa? AU huko juu alikutana na waislamu wenzie?
 
Kwahiyo huko mbele alikoendelea alisomea madrasa au kwa wale wale unaosema walikuwa na lengo la kumkatisha tamaa? AU huko juu alikutana na waislamu wenzie?
Haha! Unajua hapa haturuhusu kabisa maswali magumu!
 
MAENDELEO NI PAMOJA NA KUBADILI MTIZAMO.
Ndugu zanguni,
Nimesoma huko nyuma post zilizojaa kejeli na kebehi hata baada ya mimi
na Ralph kufanya mjadala ambao kwangu mimi naona una mengi ya msingi
katika kulielewe tatizo linalokabili nchi yetu kwa miaka mingi.

Naamini huenda tatizo ni kuwa wengi hawajui historia ya hii nchi yetu wapi
tulikotoka na hali ilikuwaje.

Nakuombeni ndugu zangu muingie hapo chini na chukueni muda hapo kwani
kipo cha kujifunza.

Hii ni simulizi ya mkasa wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ilipodhaniwa
kalishwa chakula kilichotiwa sumu kwa nia ya kutaka kukatisha maisha yake nyumbani kwa Abdulwahid Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu katika miaka ya kati 1950 baada ya Mwalimu kutoka UNO safari ya kwanza 1955.
Mohamed Said: WOMEN LEADERSHIP SUMMIT 2018 MLIMANI CITY 27 FEBRUARY 2018
 
Ndugu yangu, kwanza nIMPONGEZE Shehe kwa JUHUDI zake katika Ilmu. Napenda pia kuwashirikisha wana Jamvi kuwa MTAZAMO kuwa ELIMU ya DARASANI NDIO Ukombozi PEKEE wa Mwanadamu, SIYO kweli kabisa (Ushahidi ni kazi alofanya Shehe kule Ubalozini haikuhitaji ELIMU ya CHETI alopata darasani). Hapa, kwa maoni yangu, HAPASWI kulaumu nafasi yake ya kwenda Sekondari na Kuona kuwa ni hasara kupangwa kusomea Ufundi......Aweke JUHUDI. Ikibidi AYAALIZE MMadarasa YOTE kwa Kujipatia Shahada ya UZAMIVU katika eneo analopenda zaidi.... Elimu HAINA MWISHO!
 
Chochote tunachokijenga kwenye misingi ya uongo kitalaaniwa. Kamwe hakiwezi kusimama
 
 
Ulalamishi tu.Sasa mbona mlisema Malina alibadilisha watainiwa wakatumia namba lakini bado performance ipo low? Nilisoma kinondoni Muslim high school tulikuwa asilimia 96 wenye shule walikuwa asilimia 4 tu.
 
Nyiokunda,

Tatizo kubwa ni wewe kutojua historia hii ambayo unajitahidi kujadili.

Inaelekea huna taarifa ya mkasa wa Shule ya Kinondoni na Kibohehe zilipofanywa kuwa seminari na kushikwana Warsha na matokeo mazuri yaliyotokea.

Nadhani pia huna taarifa kuwa ilitoka amri kutoka juu kuwa shule hizo zirejeshwe kuwa za kawaida na uongozi ulioleta maendeleo hayo ufukuzwe.

Historia hii nimeieleza hapa si muda mrefu uliopita.

Naingia Maktaba nikipata nitakuwekea.
Ingia:
Mohamed Said: BAKWATA Kibaraka (kipindi maalum)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…