Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SHEIKH HASSAN BIN AMEIR (1880 - 1979) NA WAISLAM WA BURUNDI
''Waislam walipoona juhudi zao zote hizi zinagonga ukuta wakaona waombe msaada kwa kutoka kwa ndugu zao Waislam wa Tanganyika kupitia kwa Sheikh Hassan bin Ameir.
Waislam wa Burundi wakapata msaada na wakajenga shule moja ambayo hadi leo ipo Barabara ya Nane na ya Tisa, Buyenzi na inajulikana kwa jina la Jumuiyya.
Sheikh Hassan bin Ameir alialikwa aje Burundi kuifungua shule hii na ipo hadi leo.
Katika juhudi na harakati hizi taatifa za kikachero zikafikishwa serikalini kuwa Sheikh Hassan bin Ameir kutoka Tanganyika ndiye aliyekuwa akiwachochea Waislam wa Burundi dhidi ya Wabelgiji.
Haiyumkini kabisa kuwa Sheikh Hassan bin Ameir atakuwa kaingiliana na watu wa Rwanda kwa kiasi ile ikawa yeye hawaelezi hali ya siasa ya Tanganyika na vipi Warundi kwa kiasi kile cha kuwawezesha kujenga shule asiwafunze na mbinu za siasa za mapambano.
Uhusiano huu wa Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam wa Burundi uliwatia hofu Wabelgiji kuwa kuna uwezekano mkubwa sana kwa Waislam wa Burundi wakajiunga na Waislam wenzao wa Tanganyika na kwengineko katika kupambana na serikali.
Katika hali hii ya fitna viongozi wa ya Wabelgiji wakaitisha mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa wazi na kuwataka wananchi wahudhurie mkutano ule.
Yawezekana sana kuwa nia ya mkutano huu ulikuwa kuwaonya wananchi na hasa Waislam kuhusu njama zozote za kupinga serikali. Kufika mchana uwanja wa mkutano ukawa umejaa watu wakisuburi kufika kwa Gavana kuwahutubia.
Sheikh Hassan bin Ameir alikuwapo katika mkutano huu pamoja na kundi kubwa la Waislam, wake kwa waume wamekaa sehemu yao wametulia wakisubiri kuwasili kwa Gavana uwanjani pale.
Kilichotokea pale uwanjani siku ile kilikuwa hakijaonekana.
Mara msafara wa Gavana ulipoingia uwanjani kwa vishindo vyote wanawake wa Kiislam wakasimama huku wanapiga vigelele kwa sauti ya juu sana.
Uwanja mzima ulipigwa na butwaa wakiwaangalia na kuwashangaa wanawake waliojitanda vizuri waliokuwa wakipiga vigelegele kumshangilia Gavana.
Uwanja ulisisimka na waliokuwapo wakawa wamepigwa na mshagao pamoja na Gavana mwenyewe. Walikuwa hawajapata kuona kitu kama hicho kabla.
Gavana alipokaa wale wanawake wakanyamaza na wao wakakaa. Ulipita ukimya mzito watu wakitafakari kile kilichotokea pale uwanjani.
Gavana aliposimama kuzungumza kitu cha kwanza alichouliza ni kuwa wale waliokuwa wanapiga vigelegele ni nani na wametokea wapi?
Gavana akaelezwa kuwa wale ni raia wake Waislam wakiongozwa na kiongozi wao kutoka Tanganyika, Sheikh Hassan bin Ameir.
Pale pale Gavana akawashukuru kwa kumuadhimisha kwa kiasi kile na akaagiza kuwa Sheikh Hassan bin Ameir ni mtu wa Mungu yeye na watu wake wasibughudhiwe.
Vyama vya siasa vilipoanza Burundi viongozi wa vyama hivi walikuja kuwa karibu sana na TANU kutokana na msingi huu alioweka Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam hawakusita kujiunga kwa wingi katika vyama hivi.
Viongozi wa vyama hivi wakawa wanaiangalia TANU na viongozi wake kama taa ya kuwaangazi kwenye kile kiza chao chini ya Wabelgiji na walihangaika sana kutaka na wao watiwe katika ‘’Panafricanisme,’’ kama Warundi walivyoita yaani, Pan African Freedom Movement in East and Central Africa (PAFMECA).''
Huyu ndiye Mufti Sheikh Hassan bin Ameir ambae nimemtaja sana katika taazia ya Musa Kwikima nimekuleteeni kipande hiki ili mumjue alikuwa nani na nini ulikuwa mchango wake popote pale alipoiona dhulma iwe Tanganyika au nje ya mipaka ya Tanganyika.
PICHA: Shule iliyojengwa Burundi kwa msaada wa Sheikh Hassan bin Ameir katika miaka ya 1940. Majengo ya zamani na mapya ya hivi sasa.