Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SHEIKH HUSSEIN JUMA VICE PRESIDENT WA UNITED TANGANYIKA PARTY (UTP)
Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika mtu kuitwa kuwa ni UTP ni sawa la leo kuitwa gaidi.
Picha hiyo hapo chini ya kwanza inamuonyesha Mzungu Brian Willis aliyeletwa Tanganyika na Conservative Party.
Hapa anasimamia uchaguzi wa UTP.
Pembeni yake aliyekaa wa kwanza ni Sheikh Hussein Juma aliyekuwa Vice President wa UTP.
Ofisi ya UTP ilikuwa Mtaa wa Mafia ukishavuka Mtaa wa Msimbazi unaelekea Jangwani kabla hujavuka Mtaa wa Congo.
Sheikh Hussein Juma alikuwa kati ya wanazuoni wa kutajika Dar es Salaam na alibakia hivyo hadi kufa kwake.
Pia Sheikh Hussein Juma alikuwa ndiyo kiongozi mkuu wa Batetera Union, Umoja wa Wamanyema Dar es Salaam na alikuwa Imam No 1 wa Msiiti wa Manyema.
Nafasi hii alibakia nayo maisha yake yote.
Msikiti wa Manyema wanapokuwa na uchaguzi wa kuchagua maimamu kwanza waliweka jina la Sheikh Hussein Juma kuwa Imam wa Kwanza kisha ndiyo uchaguzi utafanyika.
Sheikh Hussein Juma yeye alikuwa hagombei nafasi ile na vilevile haigombewi na yeyote.
Sheikh Hussein Juma alizaliwa na ndugu yake pacha Sheikh Hassan Juma.
Sheikh Hassan Juma ni huyo kushoto kwenye picha waliyopiga pamoja.
Sheikh Hassan Juma alikuwa na shule iliyoitwa Hassanain Mtaa wa Msimbazi hapo ikisomeshwa Qur'an na masomo ya sekula.
Kwa kitendo cha nduguye Sheikh Hussen kujiunga na UTP chama hasimu na TANU wazee wa Dar es Salaam waliwatoa watoto wao katika madras hiyo na kuwapeleka katika vyuo vingine jirani.
Uadui dhidi ya madras hiyo haikuishia hapo wanafunzi waliotolewa katika chuo hicho walikuwa wakitoka shule wakijikusanya nje ya chuo hicho na kuimba nyimbo za kuikejeli UTP.