PreGE2025 TANZIA Sheikh Jabir Haidar akutwa amefariki Bumbwisudi, chanzo cha Kifo bado kitendawili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Ni wazi kabisa kwamba mtu huyo ameuawa kwa Mauaji ya kupangwa. Wapangaji wa kifo chake ni dhahiri kabisa kwamba ni hao Watu aliokuwa nao kwa mara ya mwisho kabisa muda mfupi kabla ya kifo chake.

Kwa haraka haraka, Jeshi la Polisi tayari limeanza kuonyesha udhaifu na uzembe mkubwa kwenye suala la Upelelezi wa awali kabisa kuhusiana na kifo Cha Mtu huyo. Tayari Polisi wameshageuka na kuwa Suspects badala ya kuwa Wapelelezi wa Kesi hiyo.

1. Je, Watu hao aliokuwa nao nyakati za mwisho kabla ya kifo chake ni akina nani hasa?
2. Mawasiliano yake ya simu yanaonyesha aliwasiliana na akina nani hasa Siku chache kabla ya kifo chake?
3. Je, Namba gani/zipi za Simu(SIM Cards) zilikuwepo online wakati Mtu huyo alipokuwa yupo na hao Watu katika nyakati za mwisho za uhai wake?
4. Je, SIM Cards hizo zimesajiliwa kwa majina gani? Kwa Sasa SIM Cards hizo zinasoma zipo wapi? Je, Wahusika tayari wamekamatwa for interogations?
5. Marafiki zake wa karibu na huyo Marehemu ni akina nani hasa?
6. Marehemu alikuwa anafanya kazi gani hasa enzi za uhai wake? Ni kazi ya Ushehe tu peke yake au alikuwa anajishughulisha na kazi gani nyingine?
7. Vipi kuhusu mahusiano yake Kati yake na ndugu zake, mwenza au wenza wake, n.k?
8. Hiyo minong'ono inayodaiwa kuwepo kuhusu Kifo chake hasa inahusiana na masuala gani hasa?
 
Kuna clip yake ilitembea wiki kadhaa alikua anazungumzia ishu ya waislamu kukalia kimya haya mambo, akasema wenzetu wanapaza sauti (akimaanisha maaskofu)
Alikua na shida ya moyo na mara kadhaa alianguka kwa shida hiyo,hayo ni kwa mujibu wa ndugu zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…