Sheikh Kaluta Amri Abeid ni nani katika historia ya taifa hili?


huyu karukia mada hata heading ya thread kaisoma kwa pupa, umetumia nguvu nyingi ukiwa off point! pole mkuu!
 
Huyu jina lake kamili ni Sheikh Kaluta Amri Abedi. Alizaliwa na ni mwenyeji wa Kigoma. Alizaliwa mwaka 1924. Alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Magharibi ukiunganisha mikoa ya Kigoma, Tabora na Shinyanga wakati wa enzi ya ukoloni. Alikuwa Meya wa kwanza mweusi wakati wa enzi za ukoloni na aliendelea na nafasi hiyo hadi siku Tanganyika ilipopata Uhuru wake hapo mwaka 1964. Baada ya Uhuru, akawa Waziri wa kwanza wa sheria katika serikali huru ya Tanganyika. Baada ya hapo akahamia kwenye wizara ya utamaduni na michezo na akawa waziri katika wizara hiyo hadi mauti yake yalipomfika mwezi wa 7 mwaka 1964.


Yeye ndiye mwandishi wa Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Sheikh K. Amri Abedi, kitabu cha kwanza kabisa kufundisha sheria za kutunga mashairi.

Alifia Ujerumani alipokwenda kutibiwa na mazishi yake yalifanyika pale Temeke ambapo viongozi wa kubwa wa bara la Afrika akiwamo Marehemu Rais Jomo Kenyatta wa Kenya walihudhuria mazishi yake. Inaaminika kifo chake kilisabibishwa na kuwekewa sumu kwenye chakula alipokwenda Misri kikazi akiwa na Nyerere pamoja na Kawawa. Hadi leo hakuna uchunguzi wowote uliofanywa na serikali ili kugundua sababu ya kifo chake.
 
Kweli hakuna kuchelewa kusoma ila fursa ya kusoma ndiyo yaweza chelewa.Nimepata bonge la shule leo.
 
msamehe bure HUYU AMECHELEWA KUJUA!!!!!!!!!!!!!!!!!! na inaonesha jinsi watanzania tusuvyokuwa watu wakupenda kujisomea na kudadisi. HUO UWANJA NI KUMBUKIZI YA SHEIKH AMRI ABEID KALUTA

Aksanteni kwa kunielewesha, Tatizo sio kuchelewa kujua, unapomuelimisha mtu huna haja ya kutumia lugha kejeli. Nchi yetu haina Historia moja, Inakuwa bahati mbaya kwa sisi wengine tulio kosa bahati ya kusoma elimu katika nchi tulio zaliwa. Sijawahi asilani kusikia hili jina AMRI ABEID KALUTA.
 

Picha hii ilipigwa Mwanzoni mwa Miaka ya 50 wakati Mtanashati huyu akiwa Masomoni katika Chuo Kikuu cha Rabwah Nchini Pakistan.

Uwanja Maarufu wa Sheikh Amri Abeid kule Arusha umepewa jina lake, ndiye aliyekuwa Meya wa Kwanza Mwafrika katika iliyokuwa Tanganyika (Sasa Tanzania Bara) Alikuwa Meya wa Mji Mzizima sasa Dar es Salaam.
 

Jiulize Kaluta Street unadhani uliitwa kwa ajili ya nani? Mtaa wa Kaluta ni huu una ambaa ambaa na Ikulu kuelekea WAMA, ni sababu yake huyu Meya wa kwanza Mwafrika DSM
 

Asante san kwa darasa hili. Siku nyingi nilikuwa najaribu kupata maelezo kuhusu hili jina hasa ul uwanja wa Arusha kuitwa kwa jina lake. Ila kuna sehemu hapo sijui kama iko sawa , ... uhuru wa Tanganyik mwaka 1964???!!!

Leo nimeongeza kidato kupitia uzi huu.
 
Jiulize Kaluta Street unadhani uliitwa kwa ajili ya nani? Mtaa wa Kaluta ni huu una ambaa ambaa na Ikulu kuelekea WAMA, ni sababu yake huyu Meya wa kwanza Mwafrika DSM
Hata Nairobi Kenya kina mtaa una jina lake uko bussy sana kwa maduka ya simu na electonics na Hardware
 
Mambo ya vijana wa MLUGO hayo kaka!NI wataalamu wa kuchanganya habari kama waziri wao si unakumbuka ile Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Zanzibar
 

Siyo kweli! Limepewa jina kwa heshima ya Gwiji wa Kiswahili Sheikh Amri Abeid Kaluta.
 

Ahsante!
Wasalimie hapo UJIJI.
 

Mzee M Said njoo utupe historia ya kweli tupu kuhusu mzee wetu huyu!
 
tafuta kitabu kiitwacho ALMASI YA AFRIKA,ameandika mtoto wake.
utapata historia nzima ya Kaluta Abeid.
 
Kiukweli nimezaliwa na kukua arusha lakini sijawahi kumjua huyu jamaa alikua nani hahahahahaah.
 
CCM imechukua viwanja vingi sana vya serikali ..
 
Aisee leo nimejua hata ile Col.Middleton rd imetokea wapi. Thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…