Huyu jina lake kamili ni Sheikh Kaluta Amri Abedi. Alizaliwa na ni mwenyeji wa Kigoma. Alizaliwa mwaka 1924. Alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Magharibi ukiunganisha mikoa ya Kigoma, Tabora na Shinyanga wakati wa enzi ya ukoloni. Alikuwa Meya wa kwanza mweusi wakati wa enzi za ukoloni na aliendelea na nafasi hiyo hadi siku Tanganyika ilipopata Uhuru wake hapo mwaka 1964. Baada ya Uhuru, akawa Waziri wa kwanza wa sheria katika serikali huru ya Tanganyika. Baada ya hapo akahamia kwenye wizara ya utamaduni na michezo na akawa waziri katika wizara hiyo hadi mauti yake yalipomfika mwezi wa 7 mwaka 1964.
Yeye ndiye mwandishi wa Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Sheikh K. Amri Abedi, kitabu cha kwanza kabisa kufundisha sheria za kutunga mashairi.
Alifia Ujerumani alipokwenda kutibiwa na mazishi yake yalifanyika pale Temeke ambapo viongozi wa kubwa wa bara la Afrika akiwamo Marehemu Rais Jomo Kenyatta wa Kenya walihudhuria mazishi yake. Inaaminika kifo chake kilisabibishwa na kuwekewa sumu kwenye chakula alipokwenda Misri kikazi akiwa na Nyerere pamoja na Kawawa. Hadi leo hakuna uchunguzi wowote uliofanywa na serikali ili kugundua sababu ya kifo chake.