Sheikh Ibrahim Kaniki amesema hakuna utengano kati ya dini na siasa, akisisitiza kuwa masuala ya kisiasa huathiri moja kwa moja maisha ya waumini wa dini, hivyo ni muhimu viongozi wa dini kushiriki katika kuombea amani, haki na viongozi wanaokumbwa na changamoto.
Akizungumza siku ya Jumamosi Julai 26, 2025 baada ya kuongoza dua maalum kwa ajili ya kumuombea heri na ulinzi Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, aliyeko rumande kwa tuhuma za uhaini na uchochezi, Sheikh Kaniki amesema:
“Ukisema siasa haihusiani na dini unakosea sana… ni sawa na kusema kwa sababu mimi ni mtu wa dini sitanunua, sitauza, sitakwenda hospitali, nitakuwepo tu – hiyo itakuwa balaa”.