Al maktoum
JF-Expert Member
- Nov 23, 2022
- 513
- 704
Assalaamu a'laykum.
Waislamu na watanzania kwa ujumla wametakiwa kupata mafunzo na mazingatio kutokana na matukio yaliyotukia miaka ya nyuma katika kile kinachotambulika kama " vuguvugu la waarabu " ( Rabiiu'l Arab ) ikiwa pamoja na tukio la mapinduzi kisha mauaji ya aliyekuwa kiongozi wa nchi ya Libya kanali Muammar Gadafi.
Hayo yamesemwa na sheikh Kassim Mafuta alipokuwa akizungumza na mamia ya waislamu waliohudhuria kwenye muhadhara wake alioutoa katika msikiti mkuu wa ijumaa Bondeni jijini Arusha jana jioni ya siku ya jumatatu ya tarehe 16 June 2025 baada ya swala ya Al maghribi.
Akizungumzia tukio la kuuawa kwa Muammar Gadafi sheikh kafafanua kwamba ni kweli rais Muammar Gadafi alikuwa mtawala jeuri na dikteta aliyeiminya demokrasia na uhuru wa maoni ikiwa pamoja na kuminya uhuru wa vyombo vya habari, pia ni kweli kwamba Muammar Gadafi aliwaua kikatili kwa kuwanyonga wale wote walioonyesha kupingana nae lakini pamoja na hayo yote kitendo cha walibya KUKOSA SUBIRA na kumpindua na kumuua Gadafi kimeleta madhara makubwa sana na majuto ya kudumu kwa wananchi wa nchi ya Libya na kila mtu mwenye akili anakubali kwamba walibya walifanya makosa makubwa sana kuwaunga mkono wanaharakati wa Al ikhwaanul Muslimiina (Muslim Brotherhood) na wengineo waliokuwa wakiungwa mkono na mataifa makubwa ya kimagharibi ambao walihamasisha uasi na mapinduzi dhidi ya serikali ya Muammar Gadafi .
Sheikh Kassim kafafanua kwamba maelekezo ya uislamu pindi wanapopata mtihani wa mtawala dhalimu ( Katili, dikteta, anayedhulumu watu mali zao na kuwaua kwa dhulma )
ni KUFANYA SUBIRA na kuzungumza na mtawala huyo kwa njia ya hekima, busara,adabu na uadilifu.
Akifafanua hadithi ya mtume Muhammad Swalla llaahu alayhi wa sallam inayosema " Jihadi bora kabisa ni kusema neno la haki mbele ya mtawala jeuri" sheikh amewaasa viongozi wa dini wanapopata nafasi ya kukutana na viongozi wa nchi kutumia nafasi hizo vizuri kuwaambia watawala ukweli juu ya malalamiko, kero, changamoto na mambo yote ambayo yanawaumiza wananchi toka serikalini na viongozi wa dini wasiwe wanafiki wanaojipendekeza kwa viongozi wa nchi kwa kuwasifu mbele yao wanapokutana nao kisha wakiwaacha na kuwapa mgongo na kurejea madhabahuni na kwenye nyumba za ibada wanaanza kuwatukana viongozi wa nchi na kufanya uchochezi kwa kuhamasisha chuki ya wananchi dhidi ya serikali yao.
Akieleza maelekezo ya uislamu juu ya kuwaheshimu na kuwatii viongozi ametoa mfano wa wazazi kwamba kama uislamu unavyohimiza kuwatii na kuwaheshimu wazazi vilevile unahimiza kuwatii na kuwaheshimu viongozi wa nchi na kwamba pale inapotokea viongozi wa nchi wamekosea yatakiwa wakosolewe kwa adabu, heshima, hekima na busara na sio kuwatukana na kuwavunjia heshima kwa kuwasema madhabahuni,na kwenye mitandao ya kijamii.
Akitoa neno la shukrani baada ya muhadhara huo sheikh mkuu (bakwata ) mkoa wa Arusha sheikh Shaban Abdallah amesema kwamba neema ya amani haina mbadala ya kwamba kuna kitu bora tutakachokipata baada ya amani kuondoka hivyo akaeleza kwamba pamoja na kwamba uislamu unakataza kumtukana mtu yeyote , kuwatukana viongozi wa nchi kama rais, makamu wa rais, waziri mkuu na wakuu wa mikoa ni jambo baya sana linalokwenda kinyume na mafundisho ya uislamu kwakuwa mtume Muhammad Swalla llaahu alayhi wa sallam anasema "kumtukana muislamu ni uasi na kumuua ni ukafiri"
Pia sheikh Shaban kawakumbusha watanzania wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kuwachagua viongozi watakaoona kuwa wanafaa muda wa kupiga kura utakapofika katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Sheikh Kassim Mafuta ambaye ni muasisi na msimamizi mkuu wa chuo cha kiislamu cha Ibin Taimiyyah kilichopo katika kata ya Pongwe jijini Tanga yupo katika ziara ya kimkakati ya siku tano katika mikoa ya kanda ya kaskazini na kanda ya kati na leo mchana Jumanne tarehe 17 June 2025 anatarajiwa kuzungumza na waislamu wa mji wa Babati mkoani Manyara baada ya swala y adhuhuri na jioni ya leo atafanya muhadhara Singida mjini kuanzia saa 01:00 jioni baada ya swala ya Al magribi hadi saa 03:00 usiku wakati wa swala ya Al Ishaa.