Sheikh Kishki amfundisha Lema Alifu kwa kijiti

Sheikh Kishki amfundisha Lema Alifu kwa kijiti

Kifo kinatenganisha watu, kinatenganisha wanyama, kwa huzuni kubwa, kwa maumivu sana.
Wanaoleta huzuni juu ya kifo ni watu na wanyama wenyewe.

Watu ndio wameamua wawe na huzuni kinapotokea kifo kama ambavyo watu hao hao ndio wameamua wawe na furaha mtoto anapozaliwa.

Hivyo kuweko kwa huzuni katika kifo hakukanushi uwepo wa Mungu kwa sababu watu wenyewe ndio wameamua.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote,
Sifa hizi za mungu umezitoa katika maandiko gani ama ni sifa umeamua kuzitunga mwenyewe ili utilie nguvu ya yale unayoyapinga ?

Naomba kujua andiko gani umetoa sifa hizi za Mungu ili isiwe tunsmuongelea Mungu kwa uzushi ?
Kuwepo kwa kifo hicho kinatuonesha Mungu huyo hayupo
Umekubali mwenyewe kwamba Mungu mwenye uwezo wote ni katika sifa zake,vipi hiki kifo si ni katika uwezo wake wa kukiweka nduo maana akaweka kifo ???

unapokubali hojs ya Mungu mwenye uwezo wote maana yake uwezo wake ndio pia umefanya kifo kiwepo na hiyo HUZUNI pia iwepo kwa sababu ya uwezo wake.


angetunusuru na kifo hiki cha huzuni kubwa
Huzuni ya kifo haijaletwa na Mungu ni watu wenyewe wameamua kuwa na huzuni ksma nilivyotangulia kusema.
 
Herbalist Dr MziziMkavu kwa nini tuiamini Quran?
Kwanini tuiamini Quran? Hebu tuiulize Qurani yenyewe itatupa jibu sahihi.

Quran
Sura 2 Al-Baqara Aya ya 2. 2. Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu. chanzo Al Baqara
Ufafanuzi zaidi huo hapa chini Hichi ndicho Kitabu kilicho kamilika, kisicho kuwa na towa, nacho ni Qur'ani tunayo iteremsha isiyo tiliwa shaka yoyote na kila mwenye akili na mwenye insafu akajua kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Wala haitilii shaka kuwa yasemwayo juu ya mambo na hukumu ni ya kweli tupu. Ndani ya Kitabu hichi upo uwongofu ulio kamilika kwa walio kuwa tayari kuitafuta Kweli, na wanajikinga na madhara na mambo ya kuwaletea adhabu.
 
Tuombe Lema afahamu hilo somo na arudi kuomba msamaha hata kwa namna ya kujitoa kimaso maso .kwani wenzake wanaotoa matamko kama hayo huwa hawaishii pazuri.
Ili asiache kauli yake ikafahamika hivyo mpaka mwisho aende sehemu ahutubie atubu kwa kusema nilieleweka vibaya sikuwa na maana ile.Hapo atakuwa amejisalimisha.
Labda kwa nguvu ya vitisho lakini kiroho hamna kitu hivi yule mhindi aliyesema imani yenu ina aya za kishetani mbona mmeshindwa kumdhuru kiroho badala yake mkaenda na bisu na bado hamjamuua,uislam ni baba wa hofu.
 
Labda kwa nguvu ya vitisho lakini kiroho hamna kitu hivi yule mhindi aliyesema imani yenu ina aya za kishetani mbona mmeshindwa kumdhuru kiroho badala yake mkaenda na bisu na bado hamjamuua,uislam ni baba wa hofu.
Hakuna bisu litakalotumika kwa Lema.Hofu tu itammaliza pole pole.Atakuwa anajuta na kwa vile anawaogopa nyinyi bado ya Mwenyezi Mungu na tayari kamkosea adabu basi atanyong'onyea na sijui uchaguzi ujao kama ataweza.Dawa aende kwa skh Kishiki akatubu.
Yeye anajua mahesabu gani kuliko mahesabu ya Mungu.
 

Ushahidi juu ya Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S.W)​

Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu mmoja wa Pekee hana Mwana na Hana Mshirika wake.
Dalili nyingi zimedhihirishwa ndani ya Qur’an katika maeneo makuu matano ambamo uchunguzi wa kina na kutafakari vikifanyika vilivyo mtu atayakinisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pasina shaka yeyote. Maeneo hayo ni haya yafuatayo;
1.Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.
2.Nafsi (Dhati) ya mwanaadamu.
3.Historia ya mwanaadamu.
4.Maisha ya mitume.
5.Mafundisho ya mitume.
1.Umbile la Mbingu na Ardhi na Vyote Vilivyomo.
Maumbile mbali mbali kama vile udongo, milima, mabonde, maji, mimea, wanyama, jua, mwezi, nyota, n.k ambavyo ni ishara kubwa inayoonyesha uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w). Ishara hizo ni hizi zifuatazo;

(a) Umbile la Mbingu na Ardhi;
Tukichunguza maumbile mbali mbali ya dunia na sayari zote jinsi yalivyoundwa na kupangika kwa namna iliyo maalum kama vile jua, mwezi, nyota, n.k ni ishara tosha kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (41:9-12), (7:54), (32:4-5), (70:4), (21:30), (46:33) na (79:30).

(b) Jua, Mwezi na Nyota;
Kuwepo kwa mfumo wa ajabu uliopangika wa Jua, mwezi na Nyota na kila kimoja kina njia yake pasina kutokea mgongano au mvurugano wa aina yeyote kati yao ni ishara kubwa za kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (6:96), (7:54), (2:29), (10:5), (14:33), n.k.

(c) Usiku, Mchana, Mwanga na Giza;
Kupatikana na kubadilishana kwa usiku na mchana, mwanga na giza ni ishara tosha za kuthibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) kwa wenye akili.
Rejea Qur’an (2:164), (3:190), (17:12) na (28:71-72).

(d) Bahari, Maziwa na Mito;
Wingi wa maji yasiyo na mfano, kutofautiana ladha yake, na kutengana kati ya maji matamu na chumvi bila ya kizuizi chochote na pia vyombo vizito na vikubwa kupita juu yake bila kuzama ni dalili nyingine ya kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (25:53), (2:264), (10:22), (14:32), (16:14), (17:66), (22:65) na (53:12).

(e) Milima na Mabonde;
Milima, majabali na mabonde ambavyo vinaifanya ardhi iwe madhubuti na isiyumbe wakati wa mitetemeko na mzunguko kati ya jua, mwezi na nyota ni ishara kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (21:31), (13:3), (15:9), (16:15), (27:61), (31:10), (50:7), (77:27), (35:27), (78:7) na (88:19).

(f)Upepo, Mawingu, Mvua, Radi na Ngurumo;
Upepo, mawingu, radi, ngurumo na mvua ni vitu vinavyofanya kazi kwa ushirikiano wa ajabu unaopelekea mvua kunyesha sehemu inayohitajika. Vyote hivi ni dalili tosha juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (10:22), (13:17), (2:19-20), (2:164) na (25:48).

(g)Matunda, Mimea na Vyakula (Riziki);
Mimea na matunda mbali mbali hustawi katika aina tofauti za udongo na kutoa mazao ambayo ni riziki (chakula) kwa viumbe hai na kila kimoja kinategemea kingine katika kustawi kwake. Hii ni ishara kwa wenye akili.
Rejea Qur’an (67:21), (11:6), (29:60), (6:95,99) na (13:4).

(h)Wanyama, Ndege na Wadudu;
Viumbe vyote hivi kutokana na kutembea, kuruka kwao na kupata kwao riziki bila ya wao kujipikia na kumiliki rasilimali yeyote, bado wanaishi bila shida yeyote. Hii ni kuonyesha kuwa ni Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye pekee anayewaruzuku.
Rejea Qur’an (16:5-7), (16:79) na (3:190-191).

2.Nafsi (Dhati) ya Mwanaadamu.
Kutokana na nafsi ya mwanaadamu mwenyewe tukichunguza na kutafakari kwa makini kuna ishara nyingi zinazoonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) kama ifuatavyo;

(a) Asili, Chanzo na mwisho wa uhai wa mwanaadamu;
Uhai, hatua alizopitia na mfumo wa maisha ya mwanaadamu, vipi na lini alianza atamaliza kuishi, nini sababu ya kifo chake na kitatokea wapi na nani anayedhibiti maisha yake yote ya kila siku, tunadhibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (2:28), (30:20-21), (22:5), (75:36-40), (23:14) na (56:81-87).

(b) Mwanaadamu kutofautiana na Wanyama;
Wanaadamu kutofautiana na wanyama kimaumbile na kimalengo, ambapo lengo la mwanaadamu ni kuwa Khalifah, na wanyama ni kumtumikia mwanaadamu. Mwanaadamu amepewa akili, uhuru, vipawa na utambuzi kinyume na wanyama.
Rejea Qur’an (2:29-30), (15:28-29), (95:4) na (16:78).

(c) Kuumbwa wanaume na wanawake na kuwa na mapenzi baina yao;
Asili ya wanaadamu wote ni moja, lakini wanatofautiana kimaumbile, kihisia na kisaikolojia. Hii ni kwa ajili ya kutegemeana, kuhurumiana na kuvumiliana kimahitaji kati yao kimwili na kisaikolojia. Zote hizi ni ishara tosha za kuwepo Allah (s.w).

(d) Mwanaadamu kutofautiana lugha, rangi, kabila na taifa;
Pamoja na wanaadamu kufanana katika viungo mbali mbali vya miili yao kama ulimi, mdomo, koromeo, n.k lakini wanazungumza lugha tofauti bila ya kufunzwa na mtu yeyote. Hii ni kuwa utofauti wao ni kwa ajili ya kujuana tu, na hii ni dalili tosha.
Rejea Qur’an (30:22) na(49:13).

(e) Kutofautiana vipaji na riziki na mgawanyo wake miongoni mwa wanaadamu;
Vipaji vya wanadamu vimetofautiana mmoja na mwingine kama vile udaktari, uhandisi, ualimu, n.k. pia upatikanaji wa riziki miongoni mwao ambao hautegemei ujanja, fani au ujuzi wa mtu bali mgao maalum ili waweze kutegemeana.
Rejea Qur’an (80:24-32).

(f) Ufanyaji kazi wa viungo vya mwili wa mwanaadamu;
Myeyusho wa chakula, mfumo wa damu na ufanyaji kazi wa figo, mapafu, n.k ni mashine za ajabu zisizohitaji utengenezaji na usimamizi wowote wa kibinaadamu. Hii ni ishara kubwa juu ya uwepo Mtengenezaji Mjuzi na Mwenye Hekima.
Rejea Qur’an (30:30).

(g) Usingizi, Umbo, sura na vazi la mwanaadamu;
Umbo au sura aliyonayo mwanadamu hana uwezo wa kuibadilisha na anaridhika nayo. Tofauti na wanyama wanaadamu wana mavazi ya kujisitiri uchi na kujikinga na baridi na pia kupata usingizi pasina yeye kutaka au kujua chanzo na mwisho wake.
Rejea Qur’an (7:26), (82:6-8), (95:4) na (45:4).

(h) Mwanaadamu kumkumbuka Mwenyezi Mungu (s.w) wakati wa matatizo;
Wakati wa matatizo mwanaadamu ni mwepesi sana kurejea na kumkumbuka Mwenyezi Mungu (s.w) na kuhitajia msaada wake, hata wale wanaokana kuwepo kwake wanakiri uwepo wake bila ujanja. Hizi zote ni ishara za kuwepo kwake.
Rejea Qur’an (6:63) na (10:90).

3.Historia ya Maisha ya Mwanaadamu.
Mchakato wa maisha na historia ya mwanaadamu tangu zama za kale hadi zama hizi umeambatana na matukio makubwa yaliyovunja na kusambaratisha falme na dola mbali mbali zilizotikisha dunia vita na majeshi. Yafuatayo ni baadhi tu ya matukio hayo;

(a) Kuangamizwa watu wa (kaumu ya) Lut, Thamud, Ad na Firauni;
Pamoja na nguvu kubwa za kijeshi na ulinzi imara waliokuwa nao watu hawa, haikuwa chochote ilipofika muda wa kuangamizwa kwao. Mwenyezi Mungu mwenye nguvu zisizokifani aliwafutilia mbali kwa kutumia majeshi yake ya upepo, maji, n.k.
Rejea Qur’an (89:6-13), (30:9), (20:128) na (22:45-46).

(b) Kuangamizwa kwa jeshi la Abraha, Gavana wa Yemen;
Abraha aliandaa jeshi kubwa la askari na tembo waliofunzwa barabara kwa ajili ya kwenda kuibomoa Al-Ka’abah (Nyumba Tukufu ya Makka), lakini alisambaratishwa na jeshi dogo na dhaifu kabisa la ndege, na hatimaye ikawa ndio mwisho wao.
Rejea Qur’an (105:1-5).

(c) Kufutika na kutoweka Viongozi na Wafalme maarufu Duniani;
Viongozi na wafalme wengi waliowahi kuitawala na kuitikisa dunia na kusababisa uharibifu, mauaji, kutokana nguvu kubwa ya kijeshi waliokuwa nayo na hata wengine kufanywa miungu. Mfano akina Hitler, Mussolini na wengineo ambao mwisho wao walifutika duniani na kushindwa kujinusuru pamoja na majeshi yao.
Rejea Qur’an (56:81-87) na (67:20).

4.Maisha ya Mitume;

Kwa kuzingatia maisha ya mitume hasa waliobainisha nadni ya Qur’an, jinsi walivyofikisha ujumbe kwa watu wao kinadharia na kimatendo ni ishara tosha juu ya uwepo wa Allah (s.w). Baadhi ya mambo hayo ni haya yafuatayo;

(a) Kuwepo na kujieleza kwao kwa watu wao kuwa wao ni mitume wa Allah (s.w);
Mitume wote walithibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w), na vile vile wote walitoa dai lilelile la kuwa wao ni mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w) ijapokuwa walikuja nyakati na sehemu tofauti.
Rejea Qur’an (7:59-61), (7:65-67), (16:36), (40:78) na (35:24).

(b) Mwenendo wao mwema kutoathiriwa na mazingira ya jamii;
Mitume wengi walizaliwa na kulelewa katika jamii za kijahili, kishirikina na kuabudu masanamu, lakini na walikuwa na mienendo na tabia nzuri isiyo kuwa na mfano katika jamii husika. Hii ni ishara kuwa yupo Mlezi na Mjuzi, naye ni Allah (s.w).
Rejea Qur’an (57:25).

(c) Miujiza kuthibitisha utume wao;
Mitume walikuja na miujiza tofauti tofauti ya kuthibitisha utume wao kwa watu wao. Kila mtume alikuja na miujiza kutoka kwa Allah (s.w) kama ishara ya kufikisha ujumbe kwa watu wake iliyokuwa tofauti na uchawi, viini macho na mazingaumbwe.
Rejea Qur’an (57:25), (28:29-32), (5:110), (15:9) na (4:82).

(d) Kuhimili na kujitoa kwao muhanga;
Mitume walikuwa wavumilivu na wenye subira dhidi ya mateso, kupigwa, kufungwa gerezani, kutiwa kizuizini au kuuawa na kupata madhila, lakini hawa kukata tama na kufikisha ujumbe wao. Hii ni yupo alikuwa anawaliwaza, naye ni Allah (s.w).
Rejea Qur’an (3:21), (3:181), (4:157-158), (21:69) na (59:8).

(e) Ujasiri wa mitume mbele ya viongozi na jamii za kishirikina;
Pamoja na vitisho na viburi vya wafalme na watawala wa kishirikina, mitume hawakumchelea mtu yeyote katika kumfikishia ujumbe wao. Hii ni ishara kuwa Mwenyezi Mungu ndiye waliokuwa wanamtegemea.
Rejea Qur’an (19:42-46) na (21:57-67).

(f) Ushindi wa mitume dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu (s.w);
Mitume na wafuasi wao walikuwa wachache, dhaifu na wanyonge mbele ya maadui wa Allah (s.w) waliokuwa wengi na wenye nguvu, lakini katika mapambano mitume na wafuasi wao ndio waliopata ushindi kwa msaada kutoka kwa Allah (s.w).
Rejea Qur’an (71:25), (7:72), (26:60-68) na (8:9-10).

(g) Mitume kutohitaji malipo kutoka kwa watu wao;
Mitume walifanya kazi ngumu na nzito bila ya kuhitajia malipo yeyote kutoka kwa watu wao kinyume na viongozi wengi ambao huhitajia malipo kwa jamii zao. Mitume walikuwa na uhakika wa kupata ujira tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pekee.
Rejea Qur’an (26:127).

5.Mafundisho ya Mitume.
Hili ni eneo jingine linaloonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) katika vipengele vifuatavyo;

(a) Umoja wa ujumbe wa mitume;
Mitume walitumwa sehemu na nyakati tofauti lakini ujumbe wao ulifanana, kila mtume alifundisha Tawhiid, lengo la kuumbwa kwao, kuwahofisha na adhabu na kuwabashiria malipo mema pia. Hii ni kuwa ujumbe wao ulitoka kwa Allah (s.w).
Rejea Qur’an (7:59, 65, 73, 85, 158), (16:36) na (19:36).

(b) Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira;
Mitume karibu wote walitokea katika jamii za kishirikina na kijahili, lakini kamwe hawakuwahi kuchanganya mafundisho yao na utamaduni wa kijahili hata kama jamii nzima ilisimama dhidi yao.
Rejea Qur’an (109:1-6).

(c) Upeo wa Elimu waliokuwa nayo Mitume;
Mitume walikuwa na upeo, fikra na hekima ya hali juu katika kutatua na kuendea mambo kuliko mtu yeyote katika jamii zao, japokuwa hawakupitia vyuo au taasisi zozote za elimu. Hii ni dalili kuwa ni Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye aliyewafunza.
Rejea Qur’an (34:10-12), (27:15-19), (43:2-3) na (25:53).

Thibitisha bila kutumia rejea za vitabu vya waarabu.
 
Wewe Ni Kafiri utawezaje kuamini kuwa Mungu yupo?Wakati wewe ni Kafiri? sitaki hoja zako zisizo kuwa na msingi wowote huna hoja ya maana kuthibisha kuwa Hakuna Mungu siwezi kushindana na Mtu kafiri asiye amini kuwa kuna Mungu wakati wewe umezaliwa na ipo siku yako utakufa ndipo utakapo juwa kama kweli yupo Mungu.Utakayo yaona huko wakati umeshakufa ndipo utatamani urudi duniani kufanya toba lakini hakuna muda tena wa kutubu adhabu ya Moto wa Jahhanamu inakusbiri upate kuingizwa Motoni na kuhukumiwa huko ukakae milele kwa kukufuru kwako .Kusema eti hakuna Mungu kazi kwako subiri siku yako ifike ndipo utajuwa ninayo yasema ni ya ukweli au maneno yangu ni ya uongo. Kazi kwao.

Bila kichaka cha kifo,hizi dini zote ni upuuzi hata wewe unaamini dini kwa sababu ya hofu juu ya kifo,upuuzi mtupu.
 
Kwanini tuiamini Quran? Hebu tuiulize Qurani yenyewe itatupa jibu sahihi.

Quran
Sura 2 Al-Baqara Aya ya 2. 2. Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu. chanzo Al Baqara
Ufafanuzi zaidi huo hapa chini Hichi ndicho Kitabu kilicho kamilika, kisicho kuwa na towa, nacho ni Qur'ani tunayo iteremsha isiyo tiliwa shaka yoyote na kila mwenye akili na mwenye insafu akajua kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Wala haitilii shaka kuwa yasemwayo juu ya mambo na hukumu ni ya kweli tupu. Ndani ya Kitabu hichi upo uwongofu ulio kamilika kwa walio kuwa tayari kuitafuta Kweli, na wanajikinga na madhara na mambo ya kuwaletea adhabu.

Nilikua nakuona mtu mwerevu kumbe mpuuzi kati ya wapuuzi,utumwa wa kidini umekuondolea uwezo wako wa akili.
 
Umeulizwa swali la kudhalilisha ubongo wako, nawe ukaingia kichwakichwa.

Umeandika pumba tupu
Yani mtu anakujibu kwa hoja then unarespond kirahisi tu namna hiyo bila support yoyote as if opinion yako wewe ndo judgement ya kweli na uongo!

Ikiwa wewe umeamua kutoamini hakuna binadamu anayeweza kukuaminisha. Mtume mwenyewe (SAW) aliambiwa yeye ni muonyaji tu na uongofu unatoka kwa Allah pekee.
 
Mimi ninaweza kuwa na unakika kwamba barua niliyoletewa imetoka kwa mama angu kwa sababu ninamjua mama angu vizuri so sintokuwa na Shaka kwamba ujumbe huo umetoka kwake.
Hoja dhaifu kabisa! kwahiyo unatambua tu barua kutoka kwa yule unayemjua? kwani anakuwa yupo yeye mwenyewe kwenye hiyo barua? Umetoa mfano mzuri wa barua lakini umekosa kutambua vipi barua inafanya kazi. Kila mwisho wa barua huwa na jina na sahihi (wakati mwengine muhuri) unaoonesha authority ya wapi hiyo barua inatoka. This is how you know that this letter is from your Mother, Uncle or a King!

Sasa basi kwa ujumbe sahihi utokao kwa Allah kwetu sisi wanadamu lazima pia unakuwa na authority ya kuthibitisha kwamba maneno hayo yanatoka kwake. Hii ndo sababu mitume walikuja na miujiza to support their message to us from Allah. It is also worth to understand that when these miracles are confirmed by eye witnesses then it's a miracle for those who saw the miracle (simply implying that the message is for them who witnessed the miracle), kwetu sisi tuliopo sasa ni story of the miracle that is confirmed by the trusted source but still it is not a miracle to us but for those who witnessed it.

Now Quran is the message and the final miracle to us katika mfano uleule wa barua ulioutoa kwa kuwa ndani yake kuna miracles zinazothibitisha source ya hiyo Quran (coming from the all knowledgeable, the creator). In it kuna scientific evidences that were only confirmed by our modern science centuries after it was revealed, in it there are some linguistic miracles that man has only been able to understand recently after the advancement of the printing press and computer based analysis (E.g. ring composition found in the the Quran and within multiple verses in it like Ayatul Qursi), you will appreciate the authenticity of the Quran more ukizingatia kwamba Quran was revealed as a spoken word and not a written book. Most amazingly it was revealed to the person who could neither read nor write (Surely it was not his invention). The best writer in the world will need to revisit his one page and sometimes delete and rewrite it several times to make sure that it is correctly written and conveying the right message in the intended style of the presentation, sasa tambua kwamba hii Quran iliposomwa na Mtume kwa watu it was just 'spoken once' to the extent of what was revealed at that time, na hapakuwa na zile "eeennnh ngoja kidogo, toa hilo neno weka hili" . This is a miracle in and of it self!

Wadamu tumepokea barua (Quran)kwa aliye tuumba (Allah), ndani yake kuna mihuri mingi (dalili) zinazothibitisha kuwa huu ujembe unatoka kwake yeye muumba wa yote. Jukumu letu ni kuisoma ili tupate muongozo.
 
Hakuna bisu litakalotumika kwa Lema.Hofu tu itammaliza pole pole.Atakuwa anajuta na kwa vile anawaogopa nyinyi bado ya Mwenyezi Mungu na tayari kamkosea adabu basi atanyong'onyea na sijui uchaguzi ujao kama ataweza.Dawa aende kwa skh Kishiki akatubu.
Yeye anajua mahesabu gani kuliko mahesabu ya Mungu.
Kwanini akatubu kwa kishki?
 
Amekuelewa,atajifanya hajakuelewa.Na ajizuie tu asiende choo kikubwa na kidogo,awe hayafanyi hayo,hapo ndio atajua kama Mungu yupo au hayupo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
That is a logical non sequitur fallacy

Kushindwa ama kuweza kujizuia choo hakuna uhusiano na kuthibitisha uwepo wa Mungu.
 
Ameshakuelewa.Ajizuie asende choo kikubwa wala kidogo,kama yeye ni mwamba.Hapo alipo choò kimembana.Madaktari na wanasayansi bingwa,wameshindwa kubadilisha mfumo wa Mungu,alivyomuumba mwanadamu ende choo,ataka asitake.
Unajuaje ama unathibitisha vipi kuwa huo mfumo wa choo umewekwa na huyo Mungu?
 
Choo kunuka kunathitisha Mungu hayupo angekuepo asinge ruhusu tuteseke na harufu mbaya ya choo. Uwepo wake ungeruhusu Kila mtu asikie harufu aipendayo kutoka kwenye choo!
Hawa watu hawaelewagi hata wanachokiongea.

Yani hawaelewi kama huwa wanajipinga
 
Adamu hakuzaliwa Adamu aliumbwa na Mungu. Adamu aliumbwa kwa udongo. Yesu alizaliwa kwa Mama bikira Maria yesu sio Mungu na wala Adamu sio Mungu wote ni Wanadamu Yesu na Adamu.
Adam alikuwa mtu wa udongo?

Yan kwenye elements zote hizi tuzijuazo leo hii, Mungu aliumba watu kwa udongo?

Kweli udongo kweli kabisa nawewe unakubali?
Kazi ipo
 
Kwanini tuiamini Quran? Hebu tuiulize Qurani yenyewe itatupa jibu sahihi.

Quran
Sura 2 Al-Baqara Aya ya 2. 2. Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu. chanzo Al Baqara
Ufafanuzi zaidi huo hapa chini Hichi ndicho Kitabu kilicho kamilika, kisicho kuwa na towa, nacho ni Qur'ani tunayo iteremsha isiyo tiliwa shaka yoyote na kila mwenye akili na mwenye insafu akajua kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Wala haitilii shaka kuwa yasemwayo juu ya mambo na hukumu ni ya kweli tupu. Ndani ya Kitabu hichi upo uwongofu ulio kamilika kwa walio kuwa tayari kuitafuta Kweli, na wanajikinga na madhara na mambo ya kuwaletea adhabu.
Hapa ndipo ujinga ulipo kwenye vitabu vya dini.
Qur'an +biblia na vingine ni the same
_20230726_105312.JPG
 
Tuombe Lema afahamu hilo somo na arudi kuomba msamaha hata kwa namna ya kujitoa kimaso maso .kwani wenzake wanaotoa matamko kama hayo huwa hawaishii pazuri.
Ili asiache kauli yake ikafahamika hivyo mpaka mwisho aende sehemu ahutubie atubu kwa kusema nilieleweka vibaya sikuwa na maana ile.Hapo atakuwa amejisalimisha.
Yani wewe poyoyo unamtishia lema unamjua lema au unamsikia tu kama unamsikia tu kamuulize sabaya yule jambaz na maguful watakupa jibu vizur,kwanza haombi msamaha na huna cha kumfanya wewe endelea kuwa brainwashed na wapuuz wenzio.
 
Back
Top Bottom