Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Sheikh machachari Kundecha Akizungumza na chombo kimoja cha habari amemsifia mkuu wa wilaya ya Ubungo kwa kutekeleza maagizo ya dini katika opeareshi yake ya kupambana na madanguro na madada poa.
Sheikh Kundecha anasema Bomboko sio anatekeleza tu maagizo ya serikali bali maagizo ya Mungu hivyo anamuombea katika kutekeleza hayo majukumu yake.
Kundecha ameitaka pia serikali kutotoa vibali vya madanguro (sina hakika kama serikali ya Tanzania inatambua au kutoa vibali vya madanguro kama anavyodai Sheikh Kundecha).
Kundecha ameenda mbali zaidi kusema hata majanga ya asili ni hukumu kutoka kwa mwenyezi mungu. Anasema "Mwenyezi Mungu anaona wenyewe mamlaka hawasimamii mambo sawasawa hivyo anatoa maangamizo".
Amesisitiza Kimbunga, maporomoko na shida mbalimbali huwa vinaathiri sehemu zenye maasi.