Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Dar es Salaam, Sheikh Mohamed Mawinda, leo Julai 5, 2025 amehutubia mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa hema jipya la Askofu Mwamposa (Arise and Shine).
Katika hotuba yake, Mawinda amesisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kulinda amani ya nchi yao, wasiiharibu wala kuruhusu wengine kuivunja. Amesema amani ni msingi wa maendeleo na ustawi wa taifa.