Sheikh Mkubwa Pakistani awachana live Wapalestina asema Israel na Jerusalem ni kwa Wayahudi pekee according to Koran

Sheikh Mkubwa Pakistani awachana live Wapalestina asema Israel na Jerusalem ni kwa Wayahudi pekee according to Koran

Mlaleo

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
14,809
Reaction score
11,825

Kiongozi mkubwa kabisa Nchini Pakistani Maulana Muhammad Khan Sherani asema kuwa uislamu unatufundisha kuwa Israel ni nchi ya Wayahudi pekee. Je, ndio mpango mpya wa mahusiano ya kibalozi kati ya Israel na Pakistani yanapoelekea na kipigiwa chapuo? Kiongozi mkubwa wa kidini ni ashapitisha maamuzi ya kulitambua taifa la Israel.​

Kiongozi mkubwa wa kidini nchini Pakistani ambaye zamani alikuwa mtungasheria nchini humo ameomba kutambuliwa kwa Taifa la Israel, na pia ameomba Waislamu duniani kote kulikubali taifa la Kiyahudi.

Maulana Muhammad Khan Sherani, ambae alishawahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la kiitikadi la Kiislamu - Bodi ya Washauri wanaoishauri Serikali na Bunge katika Sheria za Kiislam nchini Pakistani - na pia Mjumbe na Mtunga Sheria katika Baraza la Taifa kwa chama cha la Jamiat Ulema-e-Islam hadi mnamo 2018, Alitamka hayo wikiendi iliyoisha kuhusina na mafundisho ya dini ya kiislamu, Katika historia ardhi ya Israel ni kwa ajili ya Wayahudi''.

Kutokana na taarifa kutoka kwa muandishi vitabu Muingereza mwenye asili ya Pakistani Bwana Noor Dahri, siku ya Jumamosi, Sherani ameshapitisha mwanzo mpya wa kulitambua Taifa la Israel, na amewataka Waislam wote hadi wa Tanzania kukubali na kutambua haki za Wayahudi katika maeno yao.

Hii ni jambo la Kimataifa, Mimi nakubaliana katika kulitambua Taifa la Israel, Sherani alisema kutokana na hiyo taarifa ya Muandishi Vitabu.
''Msomi wa Kiislamu anahitaji kuelewa kuwa katika Kitabu cha Koran na historia inatuthibitishia kuwa ardhi ya Israel ni kwa ajili ya Wayahudi pekee. Mfalme Daudi alijenga Hekalu la Mungu katika mji wa Jerusalem kwa waisrael na sio Wapalestina''.

Dahri aliwekamo video kwenye ukurasa wake wa Tweeter aliyoyazungumza Sheikh huyo Sherani, katika lugha ya Pashto.
Shirika la Habari Urdu News lilithibitisha Taarifa ya Dahri, na kurusha hewani mahojiano ya Sherani.

Katika hayo mahojiano, Sheikh Sherani alionesha kuyashinda manong'ono ya Waarabu wa Palestina kuhusiana na historia ya Ardhi ya Waisrael na kusema. '' Kunatakiwa kuwepo kwa Taifa la Israel upande wa Magharibi na Upande Taifa la Palestina upande wa Mashariki. Sherani hakuelezea zaidi kama upande wa Mashariki Magharibi uliopakana na Mto Jordan, ambao unatenganisha Israel kutoka Maeneo wanayoishi wapelestina wengi katika Ufalme wa Nchi ya Jordan, au Maeneo yaliyotengwa katika Mkataba wa mwaka 1967 wa Mstari wa Kijani. Kama hizi Nchi Mbili zikikaa na zikiishi pamoja, hapo sasa yanini mtu mwingine aje na masharti yake,'' Sheikh Sherani aliongezea.

==========

Top Pakistani cleric: Islam teaches us that Israel belongs only to the Jews​

Is a new peace deal between Israel and Pakistan in the offing? Senior Islamic cleric endorses recognition of Israel.​


Maulana Muhammad Khan Sherani

Maulana Muhammad Khan Sherani
REUTERS

A senior Pakistani Islamic cleric and former lawmaker has called for the recognition of the State of Israel, and urged Muslims around the world to accept the Jewish state.

Maulana Muhammad Khan Sherani, who served as Chairman of Pakistan’s Council of Islamic Ideology – a body which advises the government and parliament on Islamic law – and as a lawmaker in the National Assembly for the Jamiat Ulema-e-Islam party until 2018, announced over the weekend that according to Islamic theology, the historic Land of Israel “belongs only to the Jews”.
According to a report by British-Pakistani writer Noor Dahri, on Saturday, Sherani endorsed formal recognition of the State of Israel, and said Muslims are obliged to acknowledge Jewish rights to the area.

"This is an international issue, I support recognition of Israel," Sherani said according to the report. "Educated Muslims need to understand that the Quran and history prove to us that the Land of Israel belongs only to the Jews. King David built the house of God in Jerusalem for the Israelis and not for the Palestinians."

Dahri tweeted a clip from Sherani’s statement, given in the Pashto language. Urdu News confirmed Dahri’s report, releasing an exclusive interview with Sherani. In the interview, however, Sherani seemed to qualify his criticism of Palestinian Arab claims on the historic Land of Israel, saying: "there should be an Israeli state in the western part and a Palestinian state in the eastern part." Sherani did not clarify whether the east-west boundary would run along the Jordan River, which separates Israel from the Palestinian-majority Kingdom of Jordan, or along the pre-1967 Green Line. "If the two sides are sitting together, then why should anyone else have conditions,” Sherani added.
 
Huyo Sheikh atakuwa Msunni, je Ayatollah wa Iran atakubali hili?

Wasije wakasema huyu Mzee amehongwa na mabeberu ili aupotoshe umma wa Waislamu.
 
"according to Koran" ungeweka hiyo video hapa au tupe source ya hiyo video tukaisake tuisikilize, tujue ni sura gani na aya ya ngapi iliyothibitisha huo umiliki wa Wayahudi kuliko hizi lines and paragraphs ulizoweka hapa.
 
WAYAHUDI SI WAKRISTO NA SI WAISLAM so sioni sababu ya kuwahangaikia wapumbavu kama hao.
 
WAYAHUDI SI WAKRISTO NA SI WAISLAM so sioni sababu ya kuwahangaikia wapumbavu kama hao.
Kwa hiyo ukiwa budha, mpagani, Atheist unakuwa umejiharalishia kuzulumiwa haki yako?

Kwasababu tu Okonko sio mkristo/muislam KANISA / MSIKITI inapaswa kuchukua ardhi yake kwa hila?.

Hizo dini zenu Zina nini cha ziada katika uhai wa mwanadamu?
 
kwa hiyo ukiwa budha, mpagani, Atheist unakuwa umejiharalishia kuzulumiwa haki yako?.
kwasababu tu Okonko sio mkristo/muislam KANISA / MSIKITI inapaswa kuchukua ardhi yake kwa hila?.

hizo dini zenu Zina nini cha ziada katika uhai wa mwanadamu?.
Huwa mnakosea ku bundle Imani zote as if zinaongea kitu kimoja. Hapo ndio huwa mnakosea.

Ukristo unafundisha watu wote wana haki ya kuheshimiwa kwa sababu wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Alimradi ni mtu anaoaswa kuheshimiwa.

Mwanzo 9:6
"Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu"
 
Huwa mnakosea ku bundle Imani zote as if zinaongea kitu kimoja. Hapo ndio huwa mnakosea.

Ukristo unafundisha watu wote wana haki ya kuheshimiwa kwa sababu wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Alimradi ni mtu anaoaswa kuheshimiwa.

Mwanzo 9:6
"Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu"
Ahsante kwa kunisahihisha.
 
Bwana aliposema agano lake na Baba wa Imani Nabii Ibrahim atalifanya imara kweli kweli; na kwamba mbingu na nchi zitapita kuliko yeye kuiacha Israel wengine wanakuwa hawaelewi! Mungu hutenda kazi zake kwa namna ya ajabu sana; angalia wanavyonena kwa ndimi saba kila mtu na lake!

No matter Israel ni wabaya namna gani; au wana dhambi kiasi gani ahadi ya Mungu ni kwamba Israel ni taifa lake teule - penda usipende; vimba pasuka itabaki hivyo milele. Punguza chuki; tuibariki Israel ili nasi tukapate baraka.
 
Bwana aliposema agano lake na Baba wa Imani Nabii Ibrahim atalifanya imara kweli kweli; na kwamba mbingu na nchi zitapita kuliko yeye kuiacha Israel wengine wanakuwa hawaelewi! Mungu hutenda kazi zake kwa namna ya ajabu sana; angalia wanavyonena kwa ndimi saba kila mtu na lake!

No matter Israel ni wabaya namna gani; au wana dhambi kiasi gani ahadi ya Mungu ni kwamba Israel ni taifa lake teule - penda usipende; vimba pasuka itabaki hivyo milele. Punguza chuki; tuibariki Israel ili nasi tukapate baraka.
Israel sio kwamba ni wabaya au lah... wapo kwenye kujihami ambapo mtu yeyote au Taifa lolote lanafanya pale linapotishiwa uhai wake either umshinde au akushinde but hawezi kukubali bila kijitutumua kiuwezo wake.

Tumeona Saudia akiwa vitani, Irani akiwa vitani, Iraq,n.k n.k
 
Back
Top Bottom